Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

TANZANIA siku hizi kirahisi mtu UNAHATIA bila USHAHIDI !:-(

>> Tuesday, October 12, 2010

Kuna kipindi  USHAHIDI ulihitajika kwanza,....
.... kabla jamiii haijakutia HATIANI.

Siku hizi  ukiichunguza jamiii ya TANZANIA utastukia kuwa  ,...
.... ukisingiziwa wewe ni MCHAWI  watu hawahitaji tena USHAHIDI kuchukulia MSENGENYO  kuwa ni kweli.:-(

Haki ya nani siku hizi hata kama MDADA ana TAKO KUBWA la kuzaliwa  nalo kuna waaminio katumia MCHINA hata wakigawiwa HATA nafasi ya kushikashika  na KUTOMASATOMASA kwaliti ya kubonyea kisponji ya hicho kifaa.:-(


Yani inasikitisha kwakuwa katika JAMII ya Watanzania siku hizi ,....
.....HAAMINIKI mtu.:-(
Swali:
  • Unabisha?
  • SI unaona jinsi  aitiwaye tu na mtu  hadharani kuwa ni KIBAKA awezavyo kupigwa kwa marungu na MApanga na wasio na uhakika kaiba nini au kamuibia NANI?

  • SI unaona tu hata katika SIASA   hata nikitunga tu sasa hivi MWANASIASA fulani ana UKIMWI au tu  mke wake wa kikweli ni yule HAUSI GELI wao iwezavyo kuchukuliwa kuwa ni kweli hata kama hakuna hata dalili za uhakika wa ukweli wa nisemacho?

Na haki ya nani inaweza kuaminika wewe ni MCHAWI,...
.... na KITISHACHO ni kwamba kihitajiwacho ni wewe tu KUSINGIZIWA kuwa  ushawahi kudondoka uwani kwa akina MWAKIPESILE uko uchi na UNGO WAKO hata bila USHAHIDI.:-(

Swali:
  • Unabisha?Labda ni  kweli kuwa TANZANIA maisha ni magumu  KIMPWITOMPWITO ambayo yamefanya watu waiwe na imani tena na mambo,....
.... lakini labda itakuwa ni kurahisisha sana SWALA kama tusipoangalia uwezekano kuwa:

  • UMASIKINI
  • Udhaifu KIELIMU
  • na BILA kuruka  uvivu wa kufikiri kwa kuwa kufikiri ni kazi ,...

... usababishao unapata JAMII inayotapatapa kitu ambacho sasa hivi unakishuhudia  katika kuamini  CHOCHOTE bila KUKIWEKA KWENYE MZANI na ndio maana sasa hivi utakuta:

  • Makanisa mapya BWELELE  YA ajabu ajabu  kama tu DINI NYINGI  za mpaka KUABUDU KACHORI ,....
....kisa  kikisemwa  na kama ni rahisi kukisikia na kudhania umekielewa hivyo kwa WASIOFIKIRIA na KUPIMA JAMBO hugeuka ni UKWELI MTUPU,...

kama iaminiwavyo kirahisi na RAIA WEMA kuwa SHEKHE na ASKOFU wa KIPENTEKOSTE  kama tu KILUTHERI na KIKATOLIKI ni msafi ,....
.....ingawa aitiwaye MWIZI HADHARANI  yaaminika  ni kweli MWIZI bila USHAHIDI.:-(

NI WAZO tu HILI MHESHIMIWA na naliacha huku nikilitemea mate POO!
Bob Marley arudie-Running AWAY na CRAZY BALDHEAD


Peter Tosh aingilie kati tena na kushusha -Burial


Bunny WAILER asawazishe kwa kuongelea -Black HEART MANAu tu BUNNY WAILER amalizie tu kwa kutia moyo tena katika -RISE and SHINE

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Mzee wa Changamoto 1:03 am  

Duh!!

Yasinta Ngonyani 9:54 am  

Nanukuu "Yani inasikitisha kwakuwa katika JAMII ya Watanzania siku hizi ,....
.....HAAMINIKI mtu.:-(" Mwisho wa kunukuu. Hakika ni kweli dunia imeharibika sijui ndo kiama??

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP