Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Profesa Joseph L . MBELE anaendelea kuwa MWALIMU kwangu WIKI HII!

>> Wednesday, October 20, 2010

Ndani ya wiki hii nategemea kumaliza vitabu vyake vyote nivijuavyo.
Namaliza na hivi hapa pichani.:-(














Unaweza kumpata HAPA

















Kuna Mabloga wa Tanzania kadhaa navilenga vitabu vyao akiwemo Jeff Msangi ,NN MHANGO na Kamala Luta.

Tuko PAMOJA!

10 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

malkiory 3:59 pm  

Pongezi Kitururu kwa kuwa na urafiki wa karibu na vitabu.

Simon Kitururu 4:12 pm  

@Mkuu Malkiory: Nawasiwasi urafiki na vitabu wangu unawezatokana na kujisikia Mjinga.:-(

John Mwaipopo 4:42 pm  

tena u-mjinga hasa kusoma vitabu

Mbele 7:32 pm  

Ndugu Kitururu, shukrani kwa kuniweka hapa kwenye blogu yako. Furaha ya mwandishi yeyote ni kujua kuwa watu wanasoma anachoandika.

Furaha yangu nyingine ni kuwasaidia wengine wanaowazia kuandika vitabu au wamo katika kuandika. Ingawa nami nimo katika kujifunza, napenda kuwamegea wengine yale ambayo tayari nimejifunza. Tuwe na waandishi wengi, na tuwe na vitabu vingi. Ndio ndoto yangu.

Nimecheka jinsi wewe na ndugu Mwaipopo mnavyojibizana kuhusu ujinga wa (au na) kusoma vitabu. Nami napenda kuwamegeeni kauzoefu kangu.

Niliporudi Tanzania mwaka 1986 nikitokea masomoni huku Marekani, nilikuwa na shehena kubwa ya vitabu, kwani nilijua kuwa kazi yangu ya ualimu pale Chuo Kikuu Dar ilihitaji niwe na hivi vitabu.

Nilipoingia Tanzania, watu walinishangaa kwa kuleta vitabu badala ya "pick up." Ndio kusema, kwa vigezo vya wa-Tanzania, mimi ni kamanda wa wajinga :-)

emu-three 3:13 pm  

Vitabu ni rafiki mkuu wa binadamu, na ukiwa navyo hupati shiida, unaweza ukafika popote ukawaona watu wa kila aina, na ukawa tajiri mkuu au masikini wa kutupwa,....

Yasinta Ngonyani 3:41 pm  

KUJUA KUSOMA NAONA FURAHA AAAAH NAONA FURAHA. Kwa kweli asiyevisoma vitabu hivyo basi achukue nafasi na kuvisoma hutajigamba:-)

Simon Kitururu 3:48 pm  

@Mr Mwaipopo: :-)
@Prof Mbele: Nashukuru kwa yote niliyojifunza kwako na nashukuru kwa kunitembelea. Na najiuliza sijui kama ungenunua Pick Up mwaka huo leo hiii ingekuwa wapi kwa kuwa naamini Vitabu ulivyovinunua Thamani yake iko pale pale na labda hata kuwa imepanda kithamani sasa hivi .
Hapo ndipo tuonapo ni jinsi gani Jamii inathaminisha vitu vya ajabu. Unaweza kukuta kuna mtu anathamini VIATU kuliko Knowledge.:-(

@emu-three: Nanukuu ``...unaweza ukafika popote ukawaona watu wa kila aina, na ukawa tajiri mkuu au masikini wa kutupwa,....`` -mwisho wa nukuu.

Ukawa tajiri MKUU au MASIKINI wa kutupwa- kuna ukweli lakini chakuzingatia kwanza ni UTAJIRI ni NINI? Umasikini ni NINI? Kwa kuwa kuna wamuonaye MADONNA na pesa zake anavyotangatanga kimaisha kuanzia katika kuhaha na chaguo la mume mpaka dini anazoangaika nazo na kuhisi ni BOMBA la MASIKINI. Na kuna waliokuwa wanamuona Mother Teressa ambaye hakuwa na chochote kama BOMBA la TAJIRI. NI hapo sasa kasheshe lilipo.:-(

Simon Kitururu 3:49 pm  

@Yasinta mtoto wa Ngonyani: Tuko Pamoja Da mpenzi!

Mbele 5:17 pm  

Ndugu Kitururu, vitabu nilivyoingia navyo Tanzania mwaka ule ni vingi sana.

Sasa, wakati nimeombwa kuja kuanzisha masomo fulani hapa St. Olaf College (Minnesota), mwaka 1990, nilimwachia vitabu hivi rafiki yangu, Profesa Mugyabuso Mulokozi, wa Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili pale Chuo Kikuu Dar.

Aliviweka kwenye ofisi moja pale, na jamaa wengi wakiingia humo wanadhani ni vitabu vya Chuo.

Kwa miaka yote hii ishirini, watu wengi pale Chuo Kikuu wamefaidika navyo, kuanzia wanafunzi, wanaosomea shahada za juu, na walimu.

Kama ningekuwa nimepeleka "pick-up," huenda ningekuwa na uwezo wa kufungua baa mbili za kuwalewesha wa-Tanzania ulabu. Ni mradi moja unaolipa sana pale Tanzania, na wasomi wanaendesha baa, badala ya maduka ya vitabu :-)

Simon Kitururu 3:28 am  

@Prof Mbele: Lakini ungeanzisha baa kuna wengi wasingefaidika kielimu. Na cha kusikitisha inasemekana WASOMI wengi wa Kitanzania huacha kusoma vitabu wakishapasi tu MTIHANI.:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP