Aliyeandika kuhusu swala la TITI labda sio HASA ni yule MTAALAMU wa MATITI!:-(
>> Saturday, October 30, 2010
Wakati unakula MLENDA,.... 
....kumbuka TU  kuna WATAALAMU WALIOKUBUHU KATIKA KUJUA ambao wako kimya,...
....wasiopata nafasi ya kuandika KIUTAALAMU WAO kuhusu MLENDA,....
...au wasiojua tu jinsi ya kusimulia KIMAANDISHI jinsi ya kupika MLENDA wakati unasikiliza AU UNAWASOMA waongeleao MLENDA.:-(
Na umsomapo Simon Kitururu akiongelea kipengele cha mwili kitumikacho sana MSALANI,....
..... kumbuka tu  kuwa kuna wataalamu ZAIDI wa jinsi ya kubana matumizi ya muda na umadhubuti wa utumiavyo kipengele huko MSALANI ambao wako kimya kwa sababu mbaimbali  zikiwemo za kawaida  kama zile za HESHIMA kwa kudhani  wakiongelea kipengele anuai  wataonekana kama SIMON kuwa si WAHESHIMIWA .
Swali:
- SI unajua labda SHEKHE YAHYA pamoja na kutoongelea zaidi BIBLIA kama aongeleavyo utabiri labda anaijua BIBLIA kuliko hata ASKOFU kadhaa za KILUTHERI katika mpekecho wa BIBLIA?
- Si umestukia kuwa labda kunauwezekano ingawa ni wanawake ndio wenye titi lenye ujazo NA UTAALAMU WA JINSI YA KUISHI NA TITI NONO wa kutosha lakini labda kuna mwanaume ndio muongeleaji titi zaidi?
Nawaza tu MKUU!
Hebu ARRESTED DEVELOPMENT warudishe ustaarabu kwa-Revolution
Walete- Tennessee
Arrested Development warudie-Mr Wendal
Au tu ARRESTED DEVELOPMENT wamalizie na-People Everyday
 
  
 
 



0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Post a Comment