Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Labda KUNA ambao HAWANA furaha mpaka wapate MTU MWINGINE au KITU KINGINE kisicho chao cha kukichukia au tu kukiona ni USHUZI!

>> Friday, October 08, 2010


Ukichunguza ,....
.... unaweza kupata MAFILINGI kuwa  kuna wengi YAO huleta maana tu kama kwao YAWENGINE ni ushuzi.:-(


Ze mfano:
  • Labda  MWENYE tabia nzuri furaha yake  katika  UPATAJI WAKE maana katika furaha zake ni kwa kuwa wengine anafikiri wana TABIA mbaya kwa hiyo yeye katika jamii anathamani zaidi .:-(


  • Labda Mkristo katika kufurahia UKRISTO wake- kunaleta maana tu pale astukiapo kuna WAISLAMU  na WENGINE wenye dini za KIGAGAGIGIKOKO  ambao afikiriao hawataenda mbinguni  kwa kuwa si WAKRISTO kitu kimleteacho faraja katika UKRISTO wake ambao anaamini ni YESU tu ndio njia ya kwenda kwenye utamu.:-(

  • Kwenye Ukristo wa KISABATO labda faraja ni kustukia kuna WAKATOLIKI , Walutheri na hata wale WALOKOLE wa KIKAKOBE ambao kwa kisabato  kuna kitu wanakosea katika mwendo wa maringo  wa kulenga mbinguni kitu kifanyacho USABATO  mtamu.:-(

  • Wenye akili kwa kuwa wanapasi MITIANI labda furaha ni kwakuwa kuna wajinga waliofeli naa ambao hata kushusha hoja kisomi hawawezi.:-(

  • Kwa KIMWANA mzuri SURA KAMA  CHUNUSI -labda faraja huletwa na uwepo wa VIMWANA wenye sura kama JIPU kitu kisababishacho Kimwana mwenye sura kama chunusi kujisikia ahueni kwa kuwa anasifiwa zaidi ya mwenye sura kama jipu na katika kuchuna buzi akaunti yake hujaa kirahisi zaidi.:-(  • Wayahudi labda huhitaji walimwengu wengine ili wajisikie kuwa wao ndio Taifa lililochaguliwa na Mungu kwa hiyo wao spesho.:-(


Ndio ,....
.... labda hakuna mwenye FURAHA  kamili kivyake kama hakuna WENGINE na vya wengine vya kunyoshea vidole,.....


.... ili kuhalalisha  kuwa vyangu vinaunafuu kitu ambacho  husaidia baadhi ya watu ndani ya kibano KUSAIDIA ombaomba mtaani ikiwa ni  MOJA YA NJIA ya kujisaidia kupata Uahueni kuwa angalau pamoja na kuwa MAISHA ni magumu lakini angalau mimi bado sijafikia  kuwa ombaomba mtaani  ingawa ni malaya kidooooogo.:-(

Swali:

  • SI kuna waonao  mgonjwa nakupata  unafuu kuwa angalau WAO ni wazima kama tu vile WEWE ukiona MZEE aliyefikia kujinyea ujisikiavyo vizuri kuwa angalau wewe bado kijana na BADO wewe  unaweza kwenda mwenyewe chooni  kushusha kilo kadhaa  za kilichowahi kuwa chakula kwa MAMA N'TILIE?
  • SI kuna MKE WA MTU akiona  MME  wa mwenziye ni MZURI zaidi  hupunguzwa faraja ya kuvumilia angalau vijambo a.k.a MASHUZI ya MME WAKE  YA KILEVI aliyelala naye kitanda kimoja baada ya huyo MME kutoka BAA na kudai kwa nguvu chakula cha usiku cha ushindi wa haraka haraka kimagoli?
Ndio,....
....labda faraja zako hutegemea sana ufikiriavyo mapungufu ya wengine hata wasiokuhusu.:-(


NI wazo tu hili MHESHIMIWA!

Hebu O'yaba walete pambio-Crazy LoveAu tu O'Yaba wadinye tu na hii pambio-Haleluyah

1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 3:42 pm  

Hakika hakuna mada niliyowahi kuisoma hapa kibarazani na kucheka kama vile nacheka na mtu mwingine kama hii. Nanukuu " Kwa KIMWANA mzuri SURA KAMA CHUNUSI -labda faraja huletwa na uwepo wa VIMWANA wenye sura kama JIPU kitu kisababishacho Kimwana mwenye sura kama chunusi kujisikia ahueni kwa kuwa anasifiwa zaidi ya mwenye sura kama jipu na katika kuchuna buzi akaunti yake hujaa kirahisi zaidi.:-( " mwisho wa kunukuu.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP