Sikiliza LABDA unaweza kuelewa, SIKILIZIA , na labda KWA HILO utapata OGAZIMU!:-(
>> Friday, October 29, 2010
[Tahadhari: Wazo katika TARALILA HII limepinda na linamapengo!:-(]
Tatizo moja LA WATU ni kuwa WANAPAPARA na,....
..... ndio maana wwanaweza kunogewa kwa papara kama WATANZANIA wawezavyo kunonogewa kwa papara na Waziri LIYATONGA MREMA kuliko,...
......Waziri MKUU MORINGE Sokoine.:-(
Swali:
- AU?
- Samahani kama huzijui siasa za Tanzania na kama hilo linakusaidia kutojua SIASA ya Liyatonga Mrema na Moringe Sokoine si nasikia sikuizi kunakitu kina itwa GOOGLE ambacho ukigoogle unaweza kujua kuwa Profesa Lipumba ni PROFESA kweli?
Kama HUNIELEWI,....
....tulia,....
...na wakati umetulia UKIKUNWA sikilizia,....
..... na akiguna SIKILIZA pia,....
...na labda KISIKILIZWACHO bila PAPARA katika MAISHA kinaweza mpaka kukuwekea wazi UDHAIFU WA DINI YAKO PIA katika tu kukuelewesha MACHACHE utakayo ELEWA au tu utakayo kuwa na moyo wa kukubali kuwa umeelewa na hayako kama uyafuatavyo kisa PAPA BENEDIKTI kasema usitumie KONDOMU,...... hata kwa kisingizio kuna kitu unajua sasa kuliko BABU YAKO kama wanasiasa wa CCM walivyojua hata kabla NYERERE hajafa kuwa kuna kitu alikuwa anawaficha kwa kuwa yeye IKULU alikuwa anaangalia BBC kwenye TV tokea enzi TANZANIA kunaaminika hakuna TV wakati wewe TANZANIA BARA KUWA NA VIDEO ilikuwa noma.:-(
SWALI:
- SI unajua ni RUKSA kutoelewa TARARILA HII inalenga hasa nini?
.....sikiliza LABDA unaweza kuelewa, SIKILIZIA , na labda KWA HILO utapata OGAZIMU!:-(
NIMEACHA !
WIKIENDI NJEMA kwa kuwa naiunganisha kiKHERI KWAKO Ijumaa hiii kwenye hiyo kitu WIKIENDI kwako MHESHIMIWA!:-(
Hebu SHAKIRA alete -LOCA
SHAKIRA arudie pia - HIPS dont lie
Au tu hebu BIG YOUTH awaulize TENA wajifanyao wajanja SIKU HIZI kuwa wakati SHUGHULI inafanyika mwanzo -Where were all dem boys
2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Kusikiliza ni DAWA.
Ni mahala ambapo MAMBO YOTE HUANZA.
Ukisikiliza unaweza kupata BUSARA na UJINGA PIA
Unajua...
Kuwa kama hutaki kitu hutakiwi kukipa nafasi ya kukisikiliza? Unajua kwanini wale wanaofanya biashara za "impromptu" kwenye malls wanakuwa hawana wateja lakini wanalotaka ni KUSIKIIZWA TUUU?
HUSHANGAI....
wale wengine hawakujui wala kukuhisi lakini wanataka uwasikilize ili wakuuzie vitu kwenye simu?
HUJAONA...
nguvu ya kusikiliza tu?
LABDA...
Ni zaidi ya OGAZIMU
NA LABDA.....
OGAZIMU ni kitu kipendwacho na kama akipataye ananufaika na kuburudika, basi afikirie kuhamisha nguvu hizo za "mnaso" kwenye mengine mema.
TATIZO...
Ni kuwa watu wanatumia nguvu hizi kutenda ya sirini
BADALA.....
ya kutenda ya sirini na nuruni.
NA LABDA....
Nililoandika silo ulilotegemea lakini kuniwaza uniwazako sasa ni kwa kuwa umenipa nafasi ya kusoma nilichoandika (ambacho ni kama umesikiliza nilichowaza)
DUH!!!! Ni wazo kibonge na wacha niachie hapa
TUONANE "NEXT IJAYO"
@Papaa Mubelwa: Mahubiri yamenuna vizuri kweli!Kifundisho mie umeniondoa UPAGANI na miye sasa mlokole!
Ningeshukuru kweli kama watu wengi wengekuwa wanatekenyeka na neno ki-DEEP namna hiyo na siyo tu kuwa na PAPARA za kusikikia na mila kumeng'enyu wanachosikiliza kuwa hata kama ni nyama ya kuchoma kuwa moja ya utamu wa waipendayo nyama ni damu isiyoiva vizuri, chumvi na labda hata pilipili kabla hata ya mazingira kuingilia kati kuwa wanaililia kwenye sherehe yakuwa wamekatwa jando.:-(
Post a Comment