Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kama tukichunguza Waheshimiwa WAHAYA walikuwa wanafikiria NINI kilicholeta uvumbuzi muhimu wa KATELERO,...

>> Friday, October 22, 2010

....  waweza STUKIA  staili hiyo ya FIKIRA inachakuigwa.

Kama tu ukichunguza ni kwanini kila MKOA Tanzania kuna WACHAGA na biashara zao kama KENYA ilivyo kuwa na WAKIKUYU na biashara zao na kulipaumakini swala la JINSI  wahahavyo ILI  tu kuhakikisha WANAJIAJIRI hata kama ni wasomile  na  KAZI ZA KUAJIRIWA WANGEPATA na kushuka UNG'ENG'E  wanashuka kama  tu  WAZENJI washukavyo KIUNGUJA  nyororo kuliko wa  wa DAR mabishororo,.....
...... katika nchi kama TANZANNIA ambayo serikali kamwe haitaweza kutoa ajira kwa wote  LABDA basi kwao kuna la KUIGWA.:-(


Swali:
  • SI unajua nchi kama MAREKANI  ajira kubwa hutolewa na wafanyabiashara  ambao  hulka zao ni kama WACHAGA Tanzania na sera nyingi za nchi hiyo ni za kujaribu kukuza uwepo wa watu wenye silika kama za KICHAGA?

Na haki ya nani UKILICHUNGUZA KABILA lako  utagundua kuna ya KUIGWA MENGI TU ingawa KWA BAHATI MBAYA  na ya kuyatolea nje kinamna kama yale ya kutahiri KIDUDE  mabinti yapigiwayo kelele yaachwe kwa sababu zihusishwanishwazo na  utamu, AFYA au tu  kwa kuwa shughuli nzimaYA KULIPIGIA KELELE SWALA inalipa watu mishahara Ki- N.G.O  iliyostukia ulaji,.....
.. bila kusahau yale ya KAMA ya BAADHI  ya WALUGURU ya KAZOPATA ya kuona ni afadhali WAHINDI au hata WAPARE wapate kuliko apate MLUGURU mwenzao,...
.....YAPO.:-(Swali:

  • AU?
Ndio,....
.....Ukichunguza  ubunifu wa WAHAYA katika  kitu chenye uhusiano na pekechapekecha kama KATELERO ,...

.... halafu ukawaza NJE YA BOKSI  na kustukia  karibu kila kitu ukifanyacho labda kina katelero yake,....

... basi labda kila kitu ujihusishanishacho nacho  kuna UTUNDU  ukikifanyia utamu utazidi zaidi na badala ya DARASANI kupata B utapata A,...
.... au badala ya kuwa mzibua vyoo wa kawaida waweza kujikuta unamiliki KAMPUNI ya kuzibua vyoo AFRIKA MASHARIKI,....


.. au tu badala ya kuwa FISADI udhulumuye WANANCHI wenzako ukawa bomba la FISADI udhulumuye WAWEKEZAJI WANYONYAJI  kwa manufaa ya WANANCHI WENZAKO  mpaka kieleweke ili WANACHI wako nao wawe wawekezaji katika nchi isiyoendelea ya MAREKANI  kama  hali halisi  itakavyojitokeza  hapo baadaye.:-(

Swali nje kidogo ya tundu:
  • SI unakumbuka uwezekano wa MAREKANI aka USA kuwa nchi inayoendelea  na SIO ILIYOENDELEA hapo baadaye  kama unakumbuka MONGOLIA enzi za Ginghis Khan, MISRI yakina Farao , hadi URENO zilishawahi kuwa ndio nchi tajiri na zilizoendelea kuliko zote kama isifikavyo MAREKANI sasa?
  • SI unajua ukifikiria NJE YA BOKSI   suluhisho la jirani la jinsi ya kuboresha VITUMBUA inaweza kukufanya WEWE ugundue jinsi ya kuboresha KEKI  kwa hiyo labda  kwa kudadisi  katelero unaweza kupata mwanga katika ugunduzi wa manukato ya kunako?
  • Si unajua karibu kila kifaa utumiacho  chanzo chake kilikuwa ni TATIZO na kwa hiyo kama unatatizo labda unamwanya wa kuwa wewe ndio MTATUZI?

Kabla hatujaachana na  KATELERO:
  • Je MHESHIMIWA umeshawahi kuifanyia utafiti hii kitu?

Basi BWANA  kama hujawahi kuifanyia UTAFITI  HII KITU na hujui maliwazo yake katika umadhubuti wa maliwazo  kwa ushirikiano wake na PEMBEJEO ZA KAZI NANIHINO  usitishike KAMA TARALILA HII HUIELEWI inalenga nini katika KUAMSHA hisia na TAFAKARI wala zisizo na uhusiano na KATELERO  ambayo mamasta wake ni WAHAYA by reputation Mheshimiwa.:-(NI WAZO TU HILI  MHESHIMIWA!:-(
Update:
  • Baada ya kusoma comment ya Papaa Mubelwa ambaye ni MUHAYA naamini neno KATELERO katika taralila yangu  HII lisomeke: KATERERO .:-(Moja kwa moja Majek FASHEK aingilie tena kati na kurudisha ustaarabu hapa kijiweni kwa kuongelea -AFRICA UNITY


Majek Fashek aendelee na -So LONG


Au tu Baaba Maal amalizie tu kwa kurudia -Yela

11 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

EDNA 11:26 am  

mmmmh! no comment

Yasinta Ngonyani 11:51 am  

Kaazi kwelikweli! sina la kusema ila naamini Kamala na Mubelwa watachangia:-)

John Mwaipopo 1:16 pm  

any tutorials/manuals?

emu-three 3:35 pm  

Nafikiri mkuu kwa mtizamo wa watangulizi wa chapuo hili darasa limetoka kapa labda kilichodokolewa ni neno moja `katerero' sijui hata mimi nimeshindwa kulipatia `mtindo wake'ni katerero au ni katelero...
Lakini ni kweli kuwa kila kabila ukichunguza sana lina `kasifa kake' ka kulitambulisha..kiutani anyway!
Usa ni taifa kubwa lenyewe latambulika kwa `utajiri' Tanzania sifa yetu ni ipi? naona nitoke kwenye mada kidogo, siunajua tena mkuu tumetoka darasani kapa, shule uliyoitoa imebakiwa watu kuguna mmmmh, mumeelewa mmmh, nimesemaje ...umesema katerero...aisee mkuu wewe mkali wa kutekenya!
Ngoja nisome tena!

Adela Dally Kavishe 4:35 pm  

hahahahahaha nimekubali

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! 4:44 pm  

duh!

SIMON KITURURU 5:47 pm  

Kwa kifupi na urahisi zaidi nilichokuwa nakilenga ni kujaribu ugusia kuwa kuna uwezekano kituchochote uhangaikacho nacho ukikitafutia staili maalumu ya kukishughulikia kama WAHAYA walivyogundua staili maalumu ya KATELERO unaweza kuongeza ujazo wa mafanikio,...
....na ukiwa mchakarikaji kama Wachaga au Wakikuyu kwa Afrika Mashariki unaweza kustukia labda huhitaji sana kuajiriwa ili mambo yawe BIEE hata kama msomi kama tu Wahindi wa Afrika Mashariki.

@Emu-Three: Kusema ukweli sijui Hii ndude kwa lugha fanisi ni Karelero au Katerero ila natumia neno Katelero kwa kuwa naamini kila mhusika anaweza kuelewa na maanisha nini na kikubwa zaidi kuna mdada wa Kihaya miaka ya nyuma aliyekuwa ananipa eneo la kujaribia hii ndude kikazi nyeti ambaye asili yake ni Kijiji cha Katerero huko Bukoba yeye alikuwa anaiita Katelero na ndio maana ninadhani labda sijakosea jina.
Ashakum si matusi!:-(

@Wote: Asanteni kwa kunisoma na kama hamkuwa waangalifu nadhani kuna kitu mmefikiria na ndio lililokuwa lengo la huu mpekecho

SIMON KITURURU 8:56 pm  

@emu-three: Nanukuu ``Tanzania sifa yetu ni ipi?´´ -mwisho wa nukuu

Swali gumu MKUU,...
.... kwa maana katika kiboxi cha majibu kama:
-Nchi ya Amani
- Nchi ya Waoga
-Nchi ya wasiojua Kingereza
-Nchi yenye wasichana wazuri kushinda wa Kiafrika magharibi
-Nchi ya Udaku
-Nchi ya wapendanao
-Nchi masikini
-Nchi ya wakombozi wa Afrika
Nchi ya Wala rushwa
-.....,......nk

nashindwa kuchagua ni kiboxi kipi nikipige TICK.:-(

Mzee wa Changamoto 8:09 pm  
This comment has been removed by the author.
Mzee wa Changamoto 8:09 pm  

Dada Yasinta aliamini ntachangia nami nafanya hivyo, japo hakusema kipi angependa nichangie.

Hahahahaaaaaaaaaaaaa
KATEREROOOOOOOO.......Hiyo inabamba.
Sijui....
labda UJIULIZE kwanini "inashika"? lakini...
ukijiuliza sababu za wewe kuandika ulivyoandika na yule kusoma alivyosoma ndio mtajua kwanini watu wanapenda "kutererereshwa" na katerero.
MNGEANZA...
kwa kuuliza maana ya neno KATERERO ili kuweza kutambia neno hili lahusianishwa na nini? ACHILIA MBALI...
sehemu ama PAHALA paitwapo hivyo, lakini pia yaweza kuhusishwa na NENO.
kwa hiyo.....
ni pa kuanzia hapo.
HIVI...
kwanini watu wanaogopa Katerero? Ama wanaogopa kupenda? Ama wanapenda lakini wanaogopa? Kama ni mbaya kwanini "inabamba" na kama inabamba kwanini inaogopwa? Kwani ni kipi cha ajabu?
TATIZO ...
hapa ni kuwa watu wanakimbia kivuli chao. Hawapendi wapendacho kijulikane jhapo wanapenda kitendwe na asiyejua.
MMMMHHHHHHHHHHH!!!!!!!!!!!...
waHaya tumeonekana wazinzi kwa kufanya kile ambacho ninyi vijana na watoto wa siku hizi mwaenda funzwa na ma-therapist ili muokoe ndoa zenu. Sisi walijua mapema atiiiii.
NA JAPO...
twasemwa kwa namna nyingine, hii ilikuwa njia muafaka ya kutunza familia. Kuji-dedicate kwa yule umpendaye.
TATIZO...
ni kuwa waliokuwa dedicated walizidi uhalisia wa waliopendwa na hata wale wa "one touch" wakataka kung'ang'ania kuendelea "kuterererwa"
Ila hakuna mbaya katika hii. Ni sehemu ya ujuzi wa nini kifanyike kutunza ndoa.
NAAAAA...
ni kwa sababu hii, tulikuwa na low rate ya divorce, tulikuwa na familia zisizioenda "kuonja" nje na ndoa zikawa na ndoa (kabla mapenzi hayajageuzwa anasa na mkomoano)

KWA UFUPI...
ni kuwa maisha ya sasa yanaendeshwa kisengelenyuma na badala ya katerero kutumika kuterera wahusika, inawahusisha na wasiohusika na matokeo yake wanaohusishwa bila ONYO hawataki kuacha na kuamua kuweka dau zaidi na pande zote zanufaika ilhali wanaotenda kwa marudio ndio wenye kuonekana wanaharibu.

Gggggrrrrrrrr!

NSHAJIPOTEZA.

Wacha nirejee kwenye utenzi wa kutenda kile kilicho mada

TUONANE NEXT IJAYO

SIMON KITURURU 5:16 pm  

@Papaa Mubelwa: DUH!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP