Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Katika MAISHA ukishafikia UPROFESA wa kunyonya TITI,...

>> Friday, October 01, 2010




... ghafla ndio unaweza kustukia unaanza kufundishwa kunywa  UJI.:-(







SWALI pembeni kidogo ya NANIHII na katikati ya NANILIU:
  • SI umeshawahi kusikia kuwa kuna aliyejulia kufanya mapenzi na kustukia kumbe HUO  ndio mwanzo wa kujifunza upya KITU KIPYA chenye hari mpya ambacho ETI ni kuishi na mimba?:-(
  • Hufikiri wakati mtoto kashakuwa BINGWA wakunyonya titi la MAMA wakati huo labda ndio ingetakiwa aachiwe aonyeshe maringo yake kisawasawa ya kunyonya vizuri zaidi kwa kuwa anakishikilia chuchu ambacho ni meno?:-(


Na katika maisha ukisha MASTA kitu kama  tu kulima MAGIMBI mengi ,...

..... wawezastukia kuwa hata katika ukulima huo  labda kuna kipya kama vile kile cha UTAYAUZAJE MAGIMBI HAYO BWELELE ndicho kinaweza kuwa kinakungojea maeneo UJIFUNZE UPYA KIPYA ambacho ni cha kibiashara zaidi  na KINAMNA hakina uhusiano wa nyororo na UKULIMA kwa mkulima wa MAGIMBI.:-(

Swali:
  •  AU?
  • SI unakumbuka unaweza kunibishia ingawa kwako kiunyororo unaona uhusiano wa chuchu ya mwanamke na DUME zima SHABIKI LA CHUCHU KWENYE TITI lisilo hitaji maziwa ?


Na kama tu MAPENZI ya mwenye uume na mwenye la kunyonyesha TITI,...
... waweza kufikiri UMEFUDHU  katika uprofesa wa  MAPENZI kwa kuwa kwa TEKINIKI za kukubaliwa penzi WEWE KIBOKO  kwa kuwa umpendaye KAKUBALI na  kadai tu na yeye naye ANAKUPENDA,...


.... mpaka ustukie BAADAYE  au baada ya kuishi kiduchu na hilo LIMPENZI kuwa KUPATA MPENZI na ulilofikiria ni PENZI ni mwanzo tu wa safari ya PENZI  MAISHANI  yenye mpaka mchanganyiko  katika MAISHA NA MPENZI  ambayo ni mapya  MACHUNGU YA MPENZI, ambayo kuna wakati yanatia wasiwasi  kuwa HIVI NI KWELI bado unampenda mpenzi, YENYE  KUBADILIKA kwa TABIA na muonekano wa ulichokipenda kwa mpenzi, YENYE  wasiwasi wa kuwa labda MAPENZI ni kusaidiana tu kwa watu wawili kupitisha siku kwa kuwa huoni maana ya mlilowahiliita penzi, YENYE kusababisha MAPENZI ni KULEA  ze MTOTOZ pamoja tu kwa kuwa NYIE WAZAZI mliwahi kuamini nyie ni WAPENZI  ze longi, au KAMA KAWAIDA ikafikia ule wasiwasi WAKAWAIDA WAWALIOWAHI KUWA WAPENZI wa KUUZA SURA  katika kushughulikia thawabu ya kulazimisha uwapo pamoja wa WEYE na MPENZI  ili jamii iendelee kuwaheshimu MFIKIRIAVYO NI HESHIMA kuwa mko katika NDOA  na katika jamii ndio penzi,....


... kitu ambacho katika mchezo mzima KIUPROFESA wa kujua MAISHA na MPENZI labda ni kigumu kuliko  TOTO hata lisilo na kichwa kama NYUNDO kujifunza kunywa uji baada ya kujulia katika mnyonyo kushikilia TITI.:-(

NIMEACHA!:-(

Hebu twende tu KAMERUNI tupate hii -MAKOSSA compilation




Charlotte Mbango arudie-KONKAI



Au tu tubaki hapahapa Kameruni KOOL BASS aingilie shughuli katika mkuno-NDOME



Au tu KOOL BASS aonyeshe maringo yake dingilidingili mpaka chini katika BEZI..

7 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 10:35 pm  

MMhh! kazi kwelikweli nilidhani nimepotea nja kumbe ni hapa kwa mt. Simon. Naona umefanya mabadiliko. samahani nimetoka nje ya somo.

Simon Kitururu 11:16 pm  

@Yasinta: Kuna tatizo lilitokea kiufundi ndiomaana SURA ina sura mpya.:-(

o'Wambura Ng'wanambiti! 11:58 am  

taralila imekaa vema ila mpaka uwe na uprofesa wa kunyonya KIDOLE ndo uielewe vema :-(

Simon Kitururu 12:42 pm  

@Kadinali CHACHA: Acha matusi weweee!:-)

Mija Shija Sayi 1:10 am  

Kitururu, sijui kwa nini huwa nafananisha staili yako ya uandishi na kile kipindi cha MAZUNGUMZO BAADA YA HABARI....,Kile kipindi kilikuwa ni kama mzaha lakini ujumbe wake ulikuwa makini sana.

Shukrani sana kaka.

EDNA 10:00 pm  

Jamani tuambize, Chacha kaupata lini UKADINALI? au mimi ndio nimepitwa na wakati?
Ya kunyonya titi ni noma MTAKATIFU.

emu-three 11:36 am  

Mhhh, nafikiri unahitaji uprofesa wa kushika kichwa, kama Mtakatifu, au wa kushika kidevu kama dada Yasinta, ili uweze kuchakachua undani wa mantiki yenyewe.
Kukubuhu kwa kujua, kwaweza kujenga usugu, kwani anyonyaye kidole sio lazima awe mtoto, lakini je huyu tutamuita profesa, wa kunyonya kidole?
Nawaza tu mkuu!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP