Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Wasiwasi na YA KESHO uathirivyo MHESHIMIWA anavyosikilizia UTAMU leo!

>> Friday, October 08, 2010

Pamoja na yote,....

..... hakuna BINADAMU mwenye uhakika na nini kitamtokea kesho ingawa twapenda kupanga ratiba na kufikiria kwakuwa nasoma leo  ntakuwa MSOMI  kesho .:-(
Ya kesho mara nyingi hufanya  tujizuie  kusikilizia utamu LEO,.....
.... kisa LABDA ni kuhofia tu kwa kusikilizia utamu maridhawa leo,...
...kesho  shughuli nzima itakuwa ni kukabiliana na wasiwasi wa UKIMWI baada ya kupata kaswende .:-(

Swali:
  • AU?
  • Si unajua kama usingeyahofia ya kesho labda leo faraja yako ingekuwa ni kumtukana BOSI WAKO  kama tu sio mwalimu wako akuzinguaye yule UAMINIYE sio MSENGE?Ya kesho ,....
.... kuna yawafanyao waishi maisha ya kutishika na kutokula uroda maishani LEO  kwa kuwa KIKRISTO kama tu KIISLAMU,....
....TAMU KUNOGA ya LEO,....
......kesho yaweza kuwa JEHANAMU.:-(

Lakini pia Ya kesho,...
... yaweza kukufanya usiende disko leo ili ujisomee kwa kuutaka utaalamu,....
....ambao kwa jinsi dunia inavyogeuka na mateknolojia yake unaweza kujikuta baada ya kufudhu UTAALAMU  unaousomea leo ,....
....wala huo utaalamu wako hauhitajiki tena  hapo kesho.:-(


Lakini pia Ya kesho,....

..... tukumbuke tu kuwa labda ndiyo ya kupayo utamu wa maisha yako ya KIPENTEKOSTE /kilokole kwa kufaidi faraja ya kuishi ukithamini ULOKOLE na tamutamu zake ambazo mara nyingi hulinda mtu NA NI BEI RAHISI KIGHARAMA ZA MAOTI PESA  ingawa labda ,....
... baada ya kufa ukastukia wala hakuna MBINGUNI   na WATU na SISIMIZI  wote wakiwa marehemu hugeuka tu udongo na HIYO  ndio mwisho wa habari hapo KESHO.:-(


Swali:
  • Unafikiri usingetishika na ya kesho leo ungefanyanini  ili ufanikishe utamu WA HALI YA JUU?
  • Kuhusu YA KESHO - hivi unauhakika hutatokwa chunusi  kwenye pua kesho?
 Na  LABDA ni kweli ,....
.... watu hutishwa kiutofauti na YA KESHO,...
.... ndio maana wenzako hawaogopi KUIBA leo kama uogopavyo, HAWAOGOPI kuwa malaya  kama uogopavyo ingawa unafikiri wafanyalo ni tamu kweli ,....

... na wengine kwa MAKUSUDI ni WAPAGANI  kitu ukiogopacho kwa kuwa weye watishika na JEHANAMU  ikiwa ni moja tu ya yote yakufanyao UWE NA ADABU  kama MAMA TERESA  hata kwa usiyo na uhakika kama ni kweli yatatokea kesho.:-(


NAACHA MAHUBIRI HAYA Mkuu!:-(
Ijumaa na WIKIENDI NJEMA Mheshimiwa!

Moja kwa moja hebu twende South Afrika Jambo arudie-Shine on brighter
Au tu Jambo aka Sipho Jonson aendelee na -No man kill another MANAu tuhame tu ili BIZ MARKIE abadili mchezo na kutekenya kwa-La dada

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 1:49 pm  

Napenda mila zetu za kiafrika ya kesho yatatokea kesho na ya leo yatatokea leo lakini ughaibuni ya mwezi wa sita mwakani tayari watu wanajua watafanya nini. Hii kwa kweli ni stress ya maisha. Nimeipenda hii mada. Ya leo ni ya leo na ya kesho ni ya kesho. Ijumaa njema nawe pia Mt. Simon.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa 3:02 pm  

ishi maisha uliyonayo sasa kwani kesho yako inaitegemea sasa yako

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP