Nachosema na UNACHOSIKIA vinaweza visiwe na uhusiano!:-(
>> Tuesday, October 26, 2010
Labda sio unachosema ndio chenye umuhimu,.....
.... kwa kuwa ni kile wanaokusikiliza wanachosikia ndicho KASHESHE!:-(
Na kwa bahati mbaya si kila asemaye cha muhimu,....
...... husikilizwa na akisemacho kutiliwa maanani moja kwa moja na ndio maana hicho hicho CHA MAANA kitu akikiongea Mama NTILIE adharauliwaye chaweza kutopewa umuhimu ingawa akikiongea hivyohivyo MANDELA kuna watu watasikiliza na kukipa umuhimu kama ubwabwa wa msibani kwa aliyezamia msibani bila KASHESHE.:-(Swali:
- SI bado kunauwezekano nilichoandika na ulichotafsiri baada ya kunisoma labda havina uhusiano?
Naendelea kuwaza....:-(
Lakini unaweza tu kujiliwaza kwa kushuhudia ulimwenguni katika SHOO BIZ ustaarabu wa watu umefikia wapi kwa kudeku hii promosheni ya Puppetry of the PENIS
Au tu cheki na Puppetry of the vagina
1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Ndio mkuu, wakati mwingine `hali' za kimaisha zinaweza zikampa `sifa'mzungumzaji hata kama akiongea utumbo. Na watu watamshangilia na hata kumsifia. Eti kwasababu ni `mtu wa watu', kijogoo, au mkuu...,
Lakini utumbo huo akiuongea akina pangu pakavu tilia mchuzi, watu watamzomea na kumwambia anatembea uchi, hata kama uchi wake upo ndani ya chupi!
Ni hayo tu mkuu
Post a Comment