Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

WAKATI natafakari kwanini inaweza kuonekana FIDEL CASTRO kawashinda WAMAREKANI lakini ushindi HUO sio wa CUBA!

>> Sunday, October 24, 2010

[Tahadhari: Naongea kimaandishi nikiwa naifikiria  pia TANZANIA na   kutafakari  ya Robert Mugabe]


Moja ya UDHAIFU wa  NCHI ZA MAGHARIBI ,...
.... ni siasa zake za uangalifu katika kutaka kuuza danganya toto  zionekane ni TAKATIFU zenye watu wazuri wenye kupenda amani  na hazina agenda  mbaya  kwa nchi nyingine.:-(

Na ukifikiria utastukia pia ,....
.... kama MAREKANI isingekuwa inajali DUNIA itaionaje nchi hiyo,...
....FIDEL CASTRO asingeshinda vita  na WALA nchi kama AFGHANISTAN , PAKISTAN  au hata LIBYA chini ya  Muammar Abu Minyar al-Qaddhāfī  zisingezingua kihivyo kwa kuwa  kirahisi tu kwa nguvu za mabomu zingefutiliwa mbali  ,...
....hasa kama MAREKANI ingekuwa inafuata mfumo wa KI -Al-Qaida wa  kama kuna wakumlipua ukilipua na wasiohusika MUNGU hana noma na hiyo ishu.

Na  watu kama FIDEL CASTRO  ni miongoni mwa watu wajuao sana MAADUI ZAO ,...
... na baada ya kujua udhaifu wa MAADUI zao ,...
.... hupatia kucheza na UDHAIFU wao.


Swali:
  • Hufikirii kuwa moja ya udhaifu au kiwapunguziacho nguvu  VIONGOZI wa magharibi  ni  DEMOKRASIA?


  • Kwani hujui KIONGOZI mwenye nguvu kabisa ambaye yuko juu ya mahakama zote za DUNIA sasa hivi ni Rais wa CHINA kutokana na kutokuwepo demokrasia na kutokuwepo awezaye kupamburua AMRI yake  ambayo hakuna  mahakama ya CHINA iwezayo kupingana nayo?
Ndio,...
.... pamoja na washabiki wa FIDEL CASTRO kustukia huyu MZEE kashinda na atakufa kama El Comandante,....
.... hivi tunauhakika ushindi wa FIDEL ni wa CUBA ambayo  wananchi wake kibano wanakiona?

Unafikiri  ushindi wa Robert Mugabe ni ushindi wa Zimbabwe?


Tukirudi Tanzania ,...
.... unafikiria nini  ukitafakari ushindi wa Marais wote waliowahikuchaguliwa TANZANI A, unafikiri ushindi wao ulikuwa ni ushindi wa TANZANIA,....


...hasa kwa kuwa kuanzia Rais Nyerere pamoja na kujua moyo wake ulikuwa mahali sahihi  bado unaweza kupata watakaodai alikuwa na udhaifu katika kujua udhaifu wa anaokabiliana nao ndani na nje ya nchi ya Tanzania?:-(


Naendelea kuwaza......Tubadili  mkao kwa kuwasikiliza Jagged Edge wakibinya jipu kwa-Walked OUTTA Heaven


Craig Mack aingilie kati na kurudia-Flava In Ya Ear
Au tu nitafakari Fela Kuti angekuwa hai leo angekuwa anafikiria nini akiusikiliza wimbo wake na ROY AYERS uitwao-2000 Blacks Got To Be Free

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP