Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Watanzania katika kujibu SALAMU ZAKO labda ni maprofesa wa UONGO!:-(

>> Wednesday, October 06, 2010

Ukimjulia hali mtu,....
..... waweza kuwa unajitakia mwenyewe UDANGANYWE.:-(
Swali:
  • SI unajua kuna MTUZ kibao ukizisalimia majibu yao ni UONGO?
  • Kwani hujawahi kushuhudia hata mahospitalini jinsi uwezavyo kukuta MTU ni MAHUTUTI kwa ugonjwa lakini ukimsabahi kimkao wa ``HABARI ZAKO!´´ jibu atakalo kupa eti ni ´´NZURI´´?

Na wakati tunaangalia uwezekano kuwa,....
.... nikikuuliza ``Mambo VIPI!´´ wakati umechacha na unasumbuliwa na minyoo ukanijibu ``POA TU KICHAA WANGU!´´ labda ni uongo ambao haudhuru sana watu wengine,...
.... bado ukweli uko pale pale kuwa mambo yako sio POA na usipoangalia waweza kufana njaa kwa kujikaza kisabuni tufikirie mambo zako ni MSWANO tu kama FISADI linalo kuibia.:-(

NI moja ya wazo tu hili MHESHIMIWA !
SIKU NJEMA!


Hebu Mario abadili kwa - Let Me Love You



Mario Winans arudie naye jiwe -I don't wanna know

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

emu-three 1:08 pm  

Kuna wengine wanasema kuna `uwongo mzuri' uwongo unaotolewa kwa mazoea ya lugha, kwa mfano
'hujamboo bwana'
'Sijambo' anayejibua yupo kitandania mahututi, lakini anasubiri nyongeza ya swali, ndipo ajielezee.
Kuna uwongo wa kujibu ili kuzua mtafaruku zaidi kwa mfano mtu akiwa na matatizo ya presha unaweza kumdanganya ili usimshitue zaidi...
Ni hilo tu mkuu

Yasinta Ngonyani 5:01 pm  

Na hivi kwa nini salamu zetu zinachukua muda mrefu sana? utakuta mtu anamsalimia mtu na anataka kujua ukoo mzima una hali gani. em3 kwa nini umdanganye mtu kwa nini tu usisema hali yangu si nzuri kuliko kuzunguka toka mbeya na basi mpaka Liuli Badala ya kuchukua meli kutoka mbeya mpaka Liuli....Nawza tu kwa sauti.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP