Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Jana ndani ya mji wa Tampere na Bloga MALKIORY MATIYA na Deo Mponda!

>> Thursday, October 28, 2010

 Katika kuhangaika naye,...
....jana nilijikuta katika mji uitwao TAMPERE ambao Bloga MALKIORY  MATIYA na DEO MPONDA  ndiko wahangaikako naye mpaka kieleweke......


Ingawa muda  ulikuwa na kibano chake kwa kuwa mie ilibidi nidandie USAFIRI  na kuanza kivyangu tena  ,....
.... kwa mara ya kwanza nilikutana uso kwa uso na BLOGA huyu ambaye  ukimtembelea kwenye blogu yake ya ; MNYONGE MNYONGENI HAKI YAKE MPENI/Forward ever BACKWARD NEVER,...

.... utajua  yuko makini.


STORI kibao na kama kawaida kujifunza kitu kulikuwepo.

Baadhi ya Picha  zilizotunguliwa   katika tukio.....

Bloga Malkiory MatiyaNguli DEO MPONDA
Ilikuwa ni furaha sana tu kukutana na ndugu hawa na NI HILO TU MKUU!

Au hebu Letta Mbulu arudie - Mahlalela
Letta Mbulu aingizie-Carry onAu tu tena Dorothy Masuka aingilie shughuli na kumwaga -Teya TEYA

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 1:59 pm  

Mikutano ya wanabloggers bado inaendelea hatimaye leo wamekutana baadhi ya waishio Tampare. Nawaonea wivu kwel...lol ni jambo zuri kwa kweli kukutana kunazidi kujenga undugu, urafiki nk

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! 4:12 pm  

safi sana hiyo! nimemiss hiyo chai kwa kweli...lol!

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) 6:29 am  

Mabloga sisi ni ndugu na huu ni uthibitisho mmojawapo. Natumaini kwamba mlikuwa na wakati mzuri na mlijadili mambo ya maana hususan mustakabali wa nchi yetu hasa wakati huu wa uchaguzi. Na hicho kinywaji (pengine ni chai tu!), basi si ajabu pointi zilikuwa zinatiririka zenyewe. Safi sana!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP