Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Binadamu WAKIZOEA KITU hupenda kuendeleza kutenda walivyozoea HATA kama walivyovizoea havifanyi kazi tena hata katika jinsi viamshavyo PENZI kama MCHUMBA ageukapo MKE!:-(

>> Saturday, October 30, 2010

Binadamu wakizoea hata kuliambia limtu ``I LOVE U!´´,....

.....wanaweza kujikuta WANAENDELEA TU KULIAMBIA limtu ``I love U´´,....
....hata kama siku hizi hawalipendi hilo LIMTU ki ``I LOVE U!´´,....
..... kisa kisa wamezoea tu na mazoea yamegeuka TABIA nyumbani wakati siku hizi ni HAUSIGELI apendwaye kuliko MKE hasa tokea HAUSIGELI ajulie KUJISOPUSOPU na kuzibua uzuri wake uliokuwa umejificha kwa KIDUME aka MME wa MTU chini ya miguu yenye MAGAGA, bonge la kikwapa na kadhalika nyingine kadhaa zilizokuwa hazina mvuto kwa kidume mwanzoni kutokana na familia KIFISADI ilivyo zoea kutafuta mahausigeli kutoka katika famili zisizojiweza ili wa MDHULUMU mfanyakazi wa ndani kwa kumpa mshahara mdogo kabla hajastuka.:-(

Swali:
  • AU?

Ndio,....
.... watu wakizoea kuweka mbolea ya chumvi chumvi kwenye shamba lao,....
..... kirahisi wataendelea kutumia mbolea ya chumvi chumvi hata wakiambiwa inaharibu udongo wa shamba lao kama tu waliozoea kupiga kavukavu wakataavyo kondomu hata wakisimuliwa stori za UKIMWI.:-(

Swali:
  • AU?

Ndio,...
..... binadamu hupenda kuendeleza walivyozoea hata kama walivyozoea havifanyi kazi tena,...
.... na labda ndio maana bado ndoa yako imedumu ukizingatia labda ulichuja utamu zamani tu ,...
.... kitunzacho uhusiano wako na MWENZI WAKO ni mazoea tu ya kuendeleza tu VILIVYOZOELEKA.:-(

Niwazo tu hili MHESHIMIWA !:-(
Jumamosi NJEMA!Hebu Snoop DOGG abadili kwa kitu-Sixx Minutes

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP