Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

NGUVU za MAWAZO ya mtu mmoja katika kufanya WATU wafuate MKUMBO !

>> Thursday, October 07, 2010

Nguvu ya MAWAZO  ya MTU MMOJA tukichukulia Mahatma Gandhi alikuwa MTU,....
...twaweza HITIMISHA kuwa mawazo ya MTU MMOJA ambaye yaweza kuwa WEWE ndiye huyo mtu,...


.....yanaweza kuwa ndio CHANGAMOTO ya wapi kimawazo wakusikilizao, KUKUSOMA au KUKUCHUNGULIA uyafanyayo hata kama wakati huo unachunguliwa husemi kitu,.....

.....katika kuwadaka watu KATIKA KITU  wafuate MKUMBO.:-(




Ndio,...
.... PAMOJA na YOTE,....
.....UMATI  wa WATU LABDA kama tu mbuzi unatabia ya KUFUATA MKUMBO,....
.... hasa kama huo MKUMBO umaarufu wake unatokana na watu katika KOMONI SENSI ZAO kuamini aliye anzisha wazo  , MAWAZO YAKE wanayaelewa ZAIDI na katika jamii yana umaarufu ufanyao iwe rahisi KUFUATA MKUMBO.


Swali:
  • SI unajua lakini matatizo ya COMMON SENSE ni udhaifu wake kwa kuwa hutegemea atumiaye COMMON SENSE anajua nini , kitu kifanyacho kwa COMMON SENSE Wamarekani huamini ni kweli MAREKANI  ni nchi bora kuliko zote na WASWISI wanaamini USWISI ni bora kuliko zote kama tu Wajapani waaminivyo wao ni bora kuliko watu wengine wote kitu ambacho labda SI KWELI  ingawa kwao  kutokana na wajuayo KOMONI SENSE ZAO zinawafanya waamini ni KWELI?

  • Si unanielewa nachotaka kusema kuhusu KOMONI SENSI ni kuwa  kuna watakao dharau MCHICHA kwa  COMMON SENSE ZAO kwa kuwa wanapenda  NYAMA huku labda AFYA zao inahitaji zaidi MCHICHA kama kuna kitu wangelijua  ambacho kingegeuza mkao wa KOMONI SENSI zao?


Naanza taralila hii UPYA......

Ndio,....
...... katika MKUMBO wa watu ukichunguza utakuta kuna KIONGOZI,.....
....anzishaye KITU kwa MAWAZO yake kabla UMATI haujafuata mkumbo inaweza kuwa ni WEWE.:-(

Na ukifuatilia MAWAZO ya WATU mmoja mmoja,....
..... unaweza kustukia NGUVU ZA MAWAZO YA MTU mmojammoja ziwezavyo kufanya UMATI ufuate mkumbo hata kwa kuangalia MAWAZO ya watu kama:

  • YESU kwenye  mkumbo wa UKRISTO na wafuasi wake.

  • Dr James Naismith kwenye MAWAZO yake ambayo yamezaa mchezo wa BASKETBALL/ mpira wa vikapu ambao labda bila yeye tusingekuwa tunajua bughuza za akina Kobe Bryant

  • Gandhi ambaye unaweza kuona makali yake kwa hata kusababisha BONGE la umati wa Wahindi kuwagomea Waingereza na nguo zao za PAMBA bila kusahau maswala ya chumvi.

  • Rais Hassan Mwinyi katika MAWAZO yaliyonyegelesha swala zima la RUKSA.

  • Raymond Albert "Ray" Kroc katika mawazo yake yaliyosababisha biashara ya akina Richard "Dick" J. McDonald na kaka yake Maurice "Mac" J. McDonald ya Macdonald's iwe moja ya aina yakusambazia watu vyakula visaidiavyo watu kunenepa ovyo DUNIANI .:-(

  • Michael Jackson katika VIDEO za MUZIKI.
  • Madonna hasa katika mawazo yake yaliyo toa mwanya wasanii wa kike kuona ni kawaida kukaa nusu uchi.
  • Mawazo ya Ndesanjo Macha katika blogu za KISWAHILI.
  • Nk...:-(


Swali:
  • SI unajua labda ni MAWAZO YAKO yatakayosaidia kuanzisha mkumbo mwingine wa watu KESHO kama tu mawazo ya MGANGA wa KIENYEJI TUSIYEMJUA alivyofanikiwa kuanzisha ujasiriamali wa kugeuza MAALIBINO kuwa bidhaa na baadhi ya watu wakafuata MKUMBO?
  • Na siunajua Tanzania kuna ambao kufuata CCM au kufuata WAPINZANI ni kitendo cha kufuata mkumbo kwa kuwa  ni mkumbo?

Na chakusikitisha ni kwamba,....
...MAWAZO YA MWANZILISHI yakisha wanogea watu na kuwafanya waingie katika MKUMBO,...


.... labda MCHANGO WA MUANZILISHI hauhitajiki tena sana kivitendo kama tu uonavyo WAKRISTO katika mikumbo yao huko makanisani wanogewavyo na alivyosema YESU ambaye kuna wasiwasi hakuwahi kuwa MKRISTO,....

....au tu kama uonavyo WENYE MADALADALA Dar-es Salaam wasivyohitaji hata kujua aliyeanzisha MADALADALA Dar-es Salaam ni nani.:-(

NAENDELEA KUWAZA........
BAADAYE Kingunge!

Ila siwezi kuondoka bila kumsikiliza MWANADADA kipenzi changu katika GITAA la BEZI ambacho ni Esperanza Spalding katika -I know U know


Esperanza aendelee na-She got to U




Na hebu tu I-Wayne aingilie shughuli kwa hili bonge la jiwe-I need her in my arms




Au I-Wayne anyuke tu tena na-Living in love

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP