Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Labda kuna sababu MAHARAGE huwa hayaoshwi kwa kutumia SABUNI!:-(

>> Tuesday, October 12, 2010

Katika usafi ,....
.... yajulikana SABUNI ni pembejeo.


Lakini katika USAFI,....
.... inajulikana pia kuwa ingaw SABUNI  inaumadhubiti katika kuhakikisha chupi ni safi  bado haifai kuoshea MCHELE kama nia  ni kusafisha mchele usiwe na pumba au tu mawe katika UBWABWA wa leo.:-(




Swali:
  • AU?

  • SI unajua katika KUSAFISHA kuna mpaka KUFUA kwakuwa MAGIMBI na CHUPI huhitaji  taaluma tofauti  kama nia ni kuhakikisha  vyote ni visafi  kinono?


Ndio,....
.....usafishaji wa SERIKALI waweza hitaji utaalamu tofauti  na usafishaji CHOO au hata soko la mitumba,......
....na pia labda ni kweli kuwa katika KUOSHA MPUNGA ukitumia SABUNI kama uitumiavyo kuosha CHOO au uchi,.....
.... kuna watakao kuwa na uhakika WEYE umechafua MCHELE.:-(

Swali zaidi kiduchu:
  • Unafikiri usafishaji wa TANZANIA BARA na ZANZIBAR ni lazima ufanane?
  • SI unajua labda kwa sasa kuisafisha CHADEMA labda inahitaji taaluma tofauti na kusafisha CCM?

Ni wazo tu hili!

Wakati tunabadili mkao R.I.P Solomon Burke aliyetutoka juzi (March 21, 1940 –  October 10, 2010)


Tumkumbuke kwa-I Can't Stop Loving You



Hebu adinye tena kitu-Everybody needs someone




AU amalizie tu kwa wimbo unifikirishao sana kinamna hasa nikifikiria maisha uitwao-Don't give up on me

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP