Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

KIBURUDISHO MURUA kwa DUME ZIMA hata kisipokuwa ni UKE!

>> Tuesday, October 05, 2010

[ Tahadhari: Kunauwezekano TARALILA HII inadalili asilimia kadhaa za ujinga !:-(]

Maisha ni magumu ,...
.... labda ndio maana kuna baadhi ya vitu  hata vya kawaida,....
.....kuna mtu hivyo ni VIBURUDISHO.:-(

Swali:
  • SI unajua hata kama kwako BIA ni kiburudisho lakini bado  kwa mwingine kiburudisho  HUWA ni soda kiutamu MIRINDA?

Na pamoja na yote kwa mwanamke,...
.... dume zima  liitwalo BABA laweza kuwa umuhimu wake zaidi  KWA MWANAMKE ingawa ni kweli ni JINGA kama ujuavyo,....
....labda ni kutokana tu na muonekano wake wa KIUHENDISAMU kama  Rais KIKWETE ,...

...na kwa HILO kwa mdada FULANI hilo dume zima jinga ni KIBURUDISHO MURUA.:-(





Swali:
  • Unafikiri UNAUHAKIKA kuwa  moja ya BURUDANI YAKO sio hiyo yako DINI ambayo siyo ya kila mtu?

Ila kumbuka tu kuwa,....
....katika BURUDANI hata za BIA ZA BURE za aliyezoea kupiga watu mizinga BAA ,...
....moja ya utamu wake LABDA ni wapi BIA  inanywewa.

Swali:
  • SI unajua BAA nzuri inaweza kukufanya uendelee kuwepo BAA hata kama unakreti nyingine za bia NYUMBANI?

  • Na si unajua kitanda kizuri  kinaweza kuwa kina mchango wake katika burudani na MKEO ingawa unaamini ni mkeo ndio KIBURUDISHO MURUA?
Ndio,...
... labda eneo huchangia ni wapi unajisikia MURUA kufanya dhambi.:-(



NImeacha hili wazo MHESHIMIWA na nalitemea mate POO!:-(


Na hebu tu Koffi OLOMIDE na Youssou Ndour waburudishe kwa nguna-Festival



Au tu Pepe Kalle aingilie shughuli kwa kukuna kipele na -LA RUMBA



Pepe Kalle aendelee kuchokonoa kifundo na jiwe-Roger Milla







Yondo Sister atoneshe kidonda  kwa-Mbuta Mutu



Au tu Koffi Olomide na Youssou Ndour wazime mkuno tena kifupi

1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 10:17 am  

"KIBURUDISHO" dUH! KAAZI KWELIKWELI

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP