Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kumbuka MTU msafi leo akiacha KUJISWAFI nyeti,....

>> Saturday, October 09, 2010

.... kwa kuwa LEO NI msafi,....
......mpe muda TU na haki ya nani  atanuka tu HUYO.:-(


Na siri ya umjuaye ambaye hujawahi kustukia akinuka,....
.....haki ya nani tena,....
...ANAJISWAFI nyeti na maeneo mengine anuai tu  HUYO.:-(

Swali:
  • SI unajua hata MWANASIASA MSAFI LEO  - siri ya kunuka KWAKE   kesho iko tu katika kitu kidogo kama tu  kuacha tu KUJISWAFI?

  • Na si unajua katika shughuli hata ya ULOKOLE ili  iendelee kukaa KILOKOLE kama ya KISWAHILINA ibakiavyo KISWAHILINA inahitaji juhudi za kila siku angalau dozi kadhaa kwa siku iliiendelee kudinda vyema?


Ndio haki ya nani tena ,....
...ukiacha KUJISWAFI naniliii , NANIHII au tu uchi,....
...... sio  siri  KIJEBA ,....
....utakuja nuka tu WEYE  .:-(


Swali:
  • SI wewe leo MSAFI?
Tukiendeleza :....


Kumbuka tu YOYOTE mchafu,...
...akijipiga kisopusopu  unaweza kukiri mwenyewe WALAHI nabata USHUNGU walakhi,....
....MUTOTO ILIYOKUWA CHAFU siku hizi  kama tu IDDI AMINI kabla hajafa ni SAFI walakhi.:-(

Na labda kumbuka  pia,....
..... KUNA UKWELI kuwa hata kazi za akina YESU  mpaka BUDA zilikuwa zinaleta maana tu katika kulenga wachafu kutokana na kujua kwao KIBUSARA kuwa,....
......MCHAFU  akistuliwa AKAJISWAFI ,.....
..... kunauwezekano akawa msafi kinoma,....

...na hakiya nani tena MKUU hapa siongelei siongelei usafi wa kikojoleo.

NIMEACHA wazo MHESHIMIWA!
JUMAMOSI NJEMA!

Hebu SAM MANGWANA moja kwa moja aingilie shughuli kwa kukuna kipele kwa kijiti-Bana Ba Cameroun
Au tu SAM MANGWANA aendelee kukuna kipele kwa-KABIBINa asiache kuchezea eneo kwa kuwa tamu kwa-Maria TEBBO
 Na asanteni wadau WOOOTE,...
..... mkiwemo hawa ambao hatukutengana juzi ya jana katika mihaho kinamna,.......
... kama picha zangu ziwakumbukavyo.


TUKO PAMOJA!1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Chediel 9:36 am  

Mzee mawazoni niambie ndugu habari za huko mzima weye..nimepita kukusabahi

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP