Ujisikiacho KUKIONGEA kwa UHURU labda unajua kila mtu anaweza KUKIONGELEA!
>> Saturday, October 16, 2010
Sio kila kitu  kijulikanacho,...
... katika kulinda UHESHIMIWA  watu huweza kuongelea ndio maana husikii sana mheshimiwa akiongelea mkundu.:-(Lakini tatizo ni kwamba kwa kutoongelea kijulikanacho,...
.... kunafanya WAHESHIMIWA wawe na dhambi  ya kuachia  PAMOJA NA MENGI MENGINE ni pamoja  na kufanya dogodogo waendelee kupata mimba  za bila mpango au tu hata UKIMWI  kwa kuwa HAWAJUI MHESHIMIWA AJUACHO hasa   kwa kuwa vitendo vizalishavyo MATUNDA HAYO kwa waheshimiwa ni vigumu kuviongelea kwa kuwa labda zahusisha sehemu za siri za MBELE za mtu ambazo KIHESHIMA mheshimiwa hupata shida kuziongelea hata kwa BINTI WAKE kama tu apatavyo shida ya kuongelea KWA DAKITARI matatizo ya  mkundu.:-(
Swali:
- Unabisha?
Na ingawa BAADHI YA USICHOONGELEA  labda kila mtu  anakijua au ANACHO tu  kama ijulikanavyo kuwa kila mtu  ana uchi ingawa hatuongelei,....
.... kuna UWEZEKANO pia usichoongea ndio SULUHISHO la YOTE ya wapigao MAKELELE katika kuongea ili kukwepa KILE KIKUBWA KIWASUMBUACHO  WALICHO KAANACHO KIMYA ambacho wamejifunza kuwa HICHO HADHARANI kama unataka kuitwa MHESHIMIWA ,.....
.... hicho huwa HAKIONGELEWI.:-(
Swali:
- SI unajua hata kama sikujui na SITA ONGELEA TUKIKUTANA bado ukweli uko palepale kuwa najua una uchi hata kama wako una sura mbaya?
- SI unajua kwa kutokuongelea bado JAMBO a.k.a SWALA lipo pale pale ?
Ndio ,...
... hata ukae kimya ili tufikirie MLOKOLE,....
.... kama una watoto  tunajua kunakitu ulifanya,.....
.... na kama ukiwafunza watoto wako kuhusu hicho LABDA unaweza kuwaepusha angalau wasipate gono na wapate MCHUMBA mwanana kwa kuwa KATIKA   ya mchumba kuna mpaka ya kuguniana ambayo  yanaumuhimu wake  uwezao kuokoa ndoa  kwa mtu kwa kuifanya iwe NDOA yenye furaha kwa kuwa waliambiwa SIRI ya kitu .:-(
Swali:
- AU?
Na labda kuna ukweli,....
.... kiongelewacho kirahisi ni kile kifikiriwacho kuwa KILA MTU anaweza kukiongea hadharani KIRAHISI,...
.... kitu kisababishacho katika MATATIZO YA BINADAMU mengi ambayo yangekuwa na majibu waziwazi  ,...
.... wajuao MAJIBU wamekaa kimya kwa kuogopa wakiongea isije kuwa ni MATUSI  bure!:-(
Ni wazo tu  hili MHESHIMIWA na usikonde!
Hebu turudi Zimbabwe Thomas Mapfumo arudie ndude-Moyo Wangu
Au turudi tena Mali Sadio Sidibe arudie-Siguiko
Au tu Samuel L Jackson abadili kwa kurudia-Stack O Lee
 
  
 Posts
Posts
 
 




0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Post a Comment