Katika YOTE mtu awezayo kuongelea,....
>> Tuesday, October 05, 2010
.... labda ni cha MUHIMU ndicho HURUKWA katika ongeleo kwa kuwa MUONGEAJI kafunzwa na jamii kuwa hicho hadharani sio chakuongea.:-(
Swali:
- Hivi jana ni mangapi ulifikiria na hukuyaongelea?
- Si unajua ujisikiacho huru kuongea usikiwe chaweza kuwa sio uwamuzi wako kwa kuwa ni JAMII imekufanya pamoja na kuona aibu kuonekana unanunua kondomu bali pia na baadhi ya majina ya viungo vya mwili wako unaogopa kuyataja kwakuwa umefudhu katika kujua kuwa hayo majina ni MATUSI?
Ndio,....
....katika YAONGELEWAYO,...
.... labda ni MUHIMU kukumbuka uwezekano wa kuwa hayo SIO YOTE muongeaji ayafikiriayo.:-(Na afikiriacho mtu kwasiri,...
...chaweza kuwa wala si siri kama tu ijulikanavyo hata kabla ya kumvulia mtu nguo kuwa kwa vyovyote vile HAKI YA NANI TENA weye una sehemu za siri.:-(
NI WAZO TU HILI MHESHIMIWA ambalo ni ruksa kuliendelezea udhaifu !
Na USIKONDE Mkuu!
Hebu BB King anyuke-How BLUE can you get
BB King aendelee na sindimba-The thrill is gone
Eric Clapton arudie mdinyo-Wonderful tonight
Au tu ngojea tu James Brown asawazishe kwa nguna-I feel GOOD I got U
0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Post a Comment