Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Amani KITANZANIA!

>> Friday, July 29, 2011

Amani KITANZANIA,...
..... labda HATA kwa Kunguru na MENDE wakiiangalia  LABDA wangeweza kuitafsiri kama WOGA.:-(

Amani KITANZANIA,...

..... labda ni HESHIMA kwa WAHESHIMIWA ambao nyumba zao zina geti kali kitu ambacho labda ni WOGA.:-(

Amani KITANZANIA,...
.... labda ni KUFANANISHA na kwa kufananisha ya TANZANIA na ya KONGO ili kutuliza WATANZANIA ili iitwe ni AMANI labda  kuna uwezekano hilo nalo ni WOGA.

Amani KITANZANIA,...
..... labda ni USHAURI kuwa ridhika na ulichonacho kidogo kwa kuwa ni BORA kuishi tu na KIDOGO  kwa kuwa kwa kutaka zaidi hali haitakuwa SHWARI kwa kuwa inamaana itahitajika WATANZANIA wasiwe na WOGA.


Swali:
  • SI inajulikana lakini kuwa mara kibao KIDOGO ni nafuu kuliko KINGI hata katika swala la punda kupenya kwenye tundu la SINDANO?
Lakini AMANI Kitanzania,...
..... hata kama haifanani na AMANI kimizani ya tafsiri ya AMANI kwenye KAMUSI ila kama WATANZANIA wanaamini hiyo ni AMANI basi labda hiyo ni AMANI na sio WOGA.

Tatizo ni:
Je hivi WATANZANIA wana AMANI kweli?

Ni wazo tu hili MKUU!

Hebu Gil Scott-Heron arudie - Work For Peace

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP