Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Atongozaye MTU/atongozwaye akifananishwa na MPENZI aliyekubali/kukubaliwa ambaye ni yuleyule MTU!

>> Wednesday, July 13, 2011

Kuna ya MTU ya KABLA,...
... na kuna ya MTU ya BAADA.


Swali:
  • Si unakumbuka MTU kabla hajaingia kwenye MAPENZI na akishakuwa kwenye PENZI ukimchunguza unaweza kukuta KATIKA HUYO MTU MMOJA kuna mambo yatoshayo kuwa ni YA watu wawili tofauti?



Watu hubadilika,....
... na watu hukua na kuathirika na wayaingiayo baada ya kuliingia hilo PENZI ,....
... kitu kiwezacho kufanya atongozaye MTU asifanane tena na yule MPENZI wa MTU baada ya kukubaliwa na kugeuka MPENZI waishiyenaye!:-(

Swali:
  • Si unajua kushabikia hata MPIRA/KABUMBU kama mshabiki kwa nje ni tofauti na kuwa MCHEZAJI kiwanjani kitu kifanyacho WENGI wataalamu waongeleao UTAALAMU kwa nje kuweza kugeuka na kuwa wachezaji wabovu ULINGONI katika MCHEZO ULEULE kitu ambacho unaweza kufikiria ni watu wawili tofauti kwa kuwa ni vigumu kuamini aliyekuwa kwa MANENO ni mtaalamu kivitendo asivyofanana na UTAALAMU aliokuwa anauongelea?

Ndio,...
....labda katika yeyote umjuaye kwa juujuu,...
.... ndani ya huyohuyo MTU kuna upande mwingine ambao huujui,...
... na labda na yeye haujui na KWENU wote ni mpaka MJUANE na labda hata kuishi pamoja ndio utastukia kama atakavyostukia yeye kuhusu wewe kwakuwa,...
.... upande mwingine wake na wako pia ni MATUNDA ya mtakavyo tu kua pamoja, KEMISTRI yenu au tu hata mazingira yatakavyo wabana na kuibua upande wa kimalaika wenu au ule tu upande ambao kiutu ni mbaya.:-(

Ni wazo tu hili MUUNGWANA!:-(


Hebu ghafla tupitie tena UGANDA ili Joanita Kawalya arudie ndude-Obulunji Bwo Sebbo



Percy Sledge apindishe kidogo na kudunga- (If Loving You Is Wrong) I Don't Want To Be Right



Au Percy Sledge amalizie tu kwa - When a Man Loves A Woman



Kabla Otis Redding hajamalizia tu kwa ~ Love Man

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP