Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Habari zako MAMA KISEBENGO!Hujambo lakini Mwanakwetu?

>> Monday, July 25, 2011

 Ni matumaini yangu HUJAMBO !

    Madhumuni ya E-MAIL  hii ni kukujulia HALI!
Pia kukuuliza kuwa hivi baada ya wajanja kugundua internet bado unapata BARUA?
Na pia hivi si ni kweli  mara nyingi  wajuliwao hali kitamaduni za Kibongobongo huwa jibu lao hata kama wamelazwa MUHIMBILI huwa majibu yao ni kuwa hawajambo na kila kitu ni shwari?

Ni hilo tu MAMA  KISEBENGO  na wasalimie wote hapo nyumbani  na pia yule  bwana wako wa siri  muuza nyanya  pale  karibu na kioski cha karibu na nyumbani kwako!
Ni mie,
- DJ KALUBANDIKA mwana BONGELADENDA!

---------------------_____________________________------------------------

Tukiacha utani:

  • Si umestukia WATANZANIA wengi majibu yao ya SALAMU yako katika miundo ambayo automatiki  majibu yake ni CHANYA hata kama mtu chamoto anakiona?
  • Na siinasemekana kuna watu LUKUKI wenye mtandao kuandika BARUA  hata za kutongoza wameanza kusahau?


Ndio,...
.... mie niko SALAMA na SHWARI kibongobongo aisee!:-(

JUMATATU NJEMA MDAU,...
.....na usimaindi kama hunidaki stirio namaanisha nini kwenye hii TARALILA!:-(
 BAAADAYE BASI MTU WANGU!


Hebu Maxi Priest adinye tena - Wild World



Maxi Priest adai ana - Believe In Love




Kabla tu huyuhuyu Maxi Priest  hajamalizia kwa- One more chance


1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

emu-three 8:18 am  

Ni kweli mkuu kwanza unajibu sijambo, halafu baadaye unaanza kulalamika kuwa naumwa kiuno....ndio hulka, hata mtu akipiga hodo kwanza unasema karibu hata kama hukutaka kumkaribisha! Utakuta mtu kashika kituu kidogo ambacho hakifai kugawana lakini kwa utamaduni wetu utamwambia mwenzako karibu...

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP