Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Njaa SOMALIA- sijui hii ndio ile kitu idaiwayo kwa ung'eng'e kuwa ni SURVIVAL of the FITTEST?:-(

>> Thursday, July 28, 2011

Yani wakati WATU wanakufa na NJAA,....

.... inadaiwa maeneo hayo hayo kuna WATU  kama wa  Harakat al-Shabaab al-Mujahideen (HSM) maarufu kama Al-Shabaab wakatazao hata misaada ya CHAKULA isiingie.

Na wakati kuna wadaio hali ngumu SOMALIA kwa ujumla ,....
.... inasemekana wako WATU wengi tu hata kwa kudaka MELI za WATU kiuharamia ,....
...... wamekuwa mamilionea/MATAJIRI wakubwa tu kwa kipimo cha AFRIKA katika kipindi hikihiki  kidhaniwacho ni cha shida.

Sasa sijui ndio tukubali tu kuwa KILA KIBANO,....
..... kinaneema kwa baadhi ya WATU na labda ukijisikia UMEKWAA kibano MAISHANI mwako na hali fulani kumbuka labda HALI hiyo ndio siri ya KUNEEMEKA kwa WENZIO?:-(

Na si inajulikana hata TANZANIA,....
...... hali ngumu ya MAISHA kwa baadhi ni stori tu wazichekizo tu kwenye TV au kuzisikia tu MAREDIONI kwa kuwa HALI HIYO NGUMU ndio chanzo cha UAHUENI wao?


NAWAZA tu hapa MKUU!:-(

Hebu David Sanborn & Group watubadili wazo kwa kutafsiri ndudeile-Try a Little Tenderness


0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP