Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kwa kuwa MSAFIRI ni KAFIRI kuna mengi hayaongelewi MSAFIRI afanyayo akitokea DAR kwenda KIGOMA!:-(

>> Saturday, July 09, 2011

Yamkutayo msafiri SAFARINI ,...
.....labda kuna sababu MSAFIRI hasimulii kila kitu!

Swali:
  • Kwani unafikiri ni wasafiri wangapi ambao ilifikia wakajisaidia vichakani au hata kuchambia ukuta ambao vipengele hivyo huviruka katika simulizi zao za safari wadaio ilikuwa shwari ya kutoka HUKU kwenda KULE?

Ndio,...
...na hata katika safari iitwayo MAISHA,...
.... kumbuka kunastori hurukwa kwanini JAKAYA Mrisho   KIKWETE kafanikiwa kisafari kufikia kuwa Rais JAKAYA Mrisho KIKWETE nawala sio kuwa kama Rais MWINYI,...
... na ukifikiri kuwa uyasikiayo tu kuhusu safari ya maisha ya Idd AMINI kama ayasimuliavyo ndiyo yalimfanya afanikiwa kufikia kuwa   Rais Idd AMINI na KIURAIS asiwe kama Rais NYERERE,...


.... unaweza kustukia UKIIGILIZIA labda huwezi kufanikiwa  ,...


...kama Rais IDD AMIN au tu hata BINTI KHALUFANI ambaye kwa kunema HAWEZEKANI,...
....kwa kuwa haki ya nani kunavipengele katika safari iliyomfikisha MTU  alipofikia hata kwa makusudi LABDA kisimulizi  huwa vimerukwa!:-(

Swali:
  • Kwani ukimsikiliza Bill GATES tajiri kuliko watu lukuki jinsi alivyofikia utajiri wake si unaweza kudhania ni kitu rahisi ingawa ushahidi unaonyesha ukiigilizia afanyavyo labda hutafanikiwa kama yeye kwa kuwa labda kuna vipengele katika SIMULIZI za safari yake ya mafanikio huwa haisemwi?
  • Si unajua kuna wadhaniwao wamefanikiwa ambao moja ya siri ya mafanikio yao hata ya walivyopata mtaji ni kutoa tako lichokonolewe kwa kijiti kitu ambacho hawakiongelei ?:-(

Ndio,..
....hata katika MAISHA bado MHESHIMIWA MSAFIRI labda ni kafiri,...
.... na katika SIMULIZI za safari zake za MAISHA labda kuna vipengele anaruka katika simulizi!:-(

Ni wazo tu hili MHESHIMIWA ,...
...........na ni RUKSA kulitemea koozi!:-(







Hebu Digable Planets waanzishe vita mpya ile - Where I'm From





Au tu Digable Planets wamalizie tu  kwa - Rebirth Of Slick (Cool Like Dat)


2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Unknown 3:47 pm  

Endelea kusonga, Usingoje kama mikono ya muda wa saa, kutafuta njia yako mwenyewe YA kukaa, wakati unakuja siku moja.

Kwa nini watu huchagua kuishi maisha yao kwa njia hii?

Simon Kitururu 2:42 pm  

@Rasta Mcharia: Natamani ningekuwa na jibu lenye uhakika!:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP