Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kwa kuwa Siri ya UTAMU wa BONGE LA MWILI ni kipengele KIDOGO tu!

>> Friday, July 08, 2011

Na siri ya PERFECTION /Mambo BARABARA ya kitu chochote kile,.......
...kwa kawaida iko kwenye michango ya  VITU vidogovidogo  tu kama  chumvi kidogo kwa pilipili   kwenye BONGE la sinia la KITIMOTO!:-(

Swali:
  • Unabisha?

Ndio,..
... haki ya nani tena,....
... hata SIRI ya UZURI wa bonge la KINYAGO KUBWA la KIMAKONDE,....
.... kwa kawaida iko kwenye USTADI wa michongo MIDOGOMIDOGO tu ifanyayo ustukie kimechongwa na MAHIRI na hata kwa kimakonde CHUCHU kimuonekano  ni CHUCHU KWELI  hata kama iko kwenye KINYAGO cha kigoli wa KIMAKONDE.:-(

Swali:
  • Kwani wewe unamchezo wa KUDHARAU mchango wa mambo madogo madogo katika JAMBO KUBWA?
  • SI unakumbuka kuwa hata siri ya ukali wa SENTENSI kubwa kiurefu hutokana na maneno madogo madogo tu yaundayo sentensi?
  • Unataka kuniambia hujastukia kuwa kuna uwezekano hata utamu wa BONGE la MWILI kuwa labda uko kwenye kipengele kama sio ufa mdogo tu?
  • Na si inakumbukwa ni vitu vidogo kama shahawa ndio siri ya uwepo wa bonge la TEMBO?


Tukiachana nahilo,...
....kwa wahusika kwenye SERIKALI ya TANZANIA,....
.... napenda kuwakumbusha kuwa mambo madogo madogo kama MALALAMIKO ya WANANCHI, ukosaji kazi wa VIJANA waaminio wanatengwa na serikali yao, Malalamishi ya WAZANZIBAR kudai nchi yao, mpaka vifo vya WAMACHINGA tukiruka mengine,...
.... ingawa kwenu wenye nguvu mnaweza kuyadharau sasa hivi kwa udogo wake  ,...
... ila kumbukeni ni chale ndogo ndogo ambazo hugeuza MTI MKUBWA kuwa KINYAGO kidogo cha KIMAKONDE!


Ni wazo tu hili WAHESHIMIWA!:-(





Hebu Sade ahamishe kwa -Love Is Found




Sade arudie-Sweetest Taboo




Au tu Sade amalizie tena kwa- Smooth Operator


4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa 9:18 am  

ni vitu vidogo tu kama ville miaka michache iliyopita ulivyokuwa kiduchu, sasa ni dume la kumzalisha mtyu

Simon Kitururu 9:36 am  

@Komandoo Kamala: SI utani aisee -vodogovidogo vinamchezo wa kukua aisee!:-(

Vinod 2:03 pm  

ni kama punje ndogo ndogo za mpunga zinavyokusanywa na kujaza bonge la gunia. Wamejisahau kwamba kasichana kadogo hatimaye kakikua kanakuwa na bonge la tako la kukutoa udenda!

Simon Kitururu 7:16 am  

@Vinod:SI ndio hapoooo!

Daima mdharau madogomadogo anaweza kudakwa bila kujiandaa kikamilifu madogomadogo yakikuwa MAKUBWA kitu ambacho anaweza kudhania kimetokea GHAFLA.:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP