Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Mwenye HAMU ya JUISI ya UKWAJU sasa hivi ukikutananaye baada ya dakika ISHIRINI.....Labda!

>> Thursday, July 14, 2011

Mpenda JUISI ya UKWAJU mwenye HAMU ya JUISI ya UKWAJU huweza kuishi bila kuonja JUISI ya UKWAJU lakini!


Na kwa bahati nzuri ,...
.... labda mengi ambayo tunahamu nayo yako tu kama ya MPENDA juisi ya UKWAJU mwenye HAMU ya JUISI ya UKWAJU ,...
.... na  KWA HIYO twaweza kuishi bila kuwanayo ,...
......na LABDA kutokuwanayo huweza kugeuka TATIZO TU tukiligeuza kuwa TATIZO.


Swali:
  • SI nasikia kuna WANAWAKE KIBAO walioolewa na MIDUME kama sisi wenye sura mbaya ambao wanahamu na MIDUME sura kama wauza sura KIMODO ambao wanaishi nasi tu bila tatizo?
  • Na kuna midume yenye hamu ya zaidi ya mwanamke mmoja ijitulizayo na mwanamke mmoja tu aliyeanza kuota ndevu kwa raha mustarehe tu?
  • Na si unajua hapa simaanishi wala kukushawishi URIDHIKE kwa kukosa yale MABYO unahamu nayo?


Ndio,...
.... inasemekana maisha ya ``HAMU nyingi ´´hata kama zile za KUDOKOA MBOGA hayazidi dakika ishirini baada ya mtu kuingiwa na hizo HAMU,...
... kwa hiyo labda baada ya DAKIKA ishirini baada ya kuingiwa na hamu ya hata kunywa POMBE ,...
... unaweza kughairisha kwenda BAA ukiamua!:-(


Swali:
  • Kwani umewahi kuchunguza hamu zako ambazo labda ni NYINGI tu KWA SIKU ukizichunguza  kwa kawaida huwa zinadumu kwa dakika ngapi?




NI wazo tu hili MHESHIMMIWA na RUKSA kulibishia,....
.... hasa kama hamu zako hata za ukoko wa mlenda MAISHA YAKE ni MIAKA!


Hebu MPONGO LOVE aingilie kati kwa-Monama Elima



Mpongo love arudie - Masikini



 Abeti Masikini ananilii kwa - Cherie Bade




Kabla  tu SIMARO MASSIYA LUTUMBA hajatuliza zaidi kwa -Faute Ya Commercant


2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

EDNA 6:10 pm  

Mmmmh haya bwana.

Simon Kitururu 6:30 am  

@Mtu wangu Edna: Mmmmh!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP