Baada ya kuzaliwa nchi ya SUDAN KUSINI -Unafikiri nchi ya ZANZIBAR itazaliwa lini?
>> Friday, July 08, 2011
Kabla nchi ya TANGANYIKA haijazaliwa tena ,...
.....na tukiacha utani;....
- Hivi VIONGOZI ambao mara nyingi hushabikia muungano wa TANGANYIKA na ZANZIBAR kwa nini wanashindwa kuuuelezea UMUHIMU wa wakionacho kwenye MUUNGANO kitu ambacho labda kingefanya watu wengi kuachana na kushuku umuhimu wa MUUNGANO wenyewe?
- Si umestukia MUUNGANO kati ya ZANZIBAR na TANGANYIKA mpaka leo inaonekana wauelewao ni wale watawala na kwa sababu wazijuazo wakielewacho hakieleweki kwa wanacnhi wengi wa kawaida TANZANIA?
- Kwanini kuna USIRISIRI mwingi katika swala hili?
Tafadhalini VIONGOZI watetezi wa MUUNGANO,...
.... uzieni wananchi wenu MUUNGANO ili waupende kama NYIE,...
.... kwani kuomba hilo ni kama wajuao ung'eng'e wasemavyo kikiulizo -Is IT asking too much?!:-(
Kumbukeni hata kama mnadhania wasioridhika na MUUNGANO ni wachache,...
Nawaza tu kwa SAUTI!
Ijumaa na WIKIENDI njema MKUU!
Hebu tu turudi BURUNDI ili Khadja Nin arudie - Sambolera
Au tu na Marcia Griffiths abadili kidogo kwa - I Shall Sing
2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Kaka Kitururu; nakuunga mkono sana kwa hiki ulichotoa leo,maana kama kizuri watuambie na kutuweka wazi ni kizuri kwa sababu hizi za msingi na kwafaida ya wote.Lakini watu wanalalamika wao wapo kimya na kung'ang'ania tuu,kila kitu kina faida na hasara je nini kimezidi kati ya hivyo?.
mimi nimefurahia ya Sudani kusini!!!
@Kaka Kitururu vipi leo mistari haija kaa sawa/kishairi? hahahhaa!!
@Rachel:Mie ni ukimya wao katika kuelezea ni kwanini tunafaidika na MUUNGANO kama kweli tunafaidika nao ndio unaniudhi!
Na mistari yako kama kawaida imekaa sawa kabisa kama mkao wakula vile mkekani!:-)
Post a Comment