Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Ukifananisha anachowaza KIBAKA na awazacho DAKITARI bingwa,....

>> Friday, July 29, 2011

 ... waweza kufananisha WAWAZACHO kwa kuwa labda wote mizizi ya kwanini hasa WANAFANYA wafanyavyo huunganishwa na UBINADAMU na MADHAIFU yake,...
..... ambayo mojawapo ni kutafuta tu TONGE!:-(

Swali:
  • Unabisha?
  • Na si unakumbuka DAKTARI anaweza kuwa ni KIBAKA?

Ndio,...
..... UKIFANANISHA,....
......... utapata tu MFANANO ingawa  kwa juujuu UWAFANANISHAO  hata KIMAVAZI unaweza kudhani ni TOFAUTI SANA kwa kuwa wamevaa chupi za rangi na HADHI tofauti  kutokana na BINADAMU waliyojifunza KUYAENZI,...
.... wakati bado labda kikubwa wote  bado ni BINADAMU,...
......na ``UBINADAMU´´ kwa BINADAMU ni KIUNGANISHI!:-(


Ni wazo tu hili MKUU!
 Ijumaa na WIKIENDI njema MHESHIMIWA!


Hebu chapuchapu Zap MAMA aanzishe kwa-MIZIKI



Zap Mama arudie-Rafiki




Zap Mama adinye tena-FURAHI


Kabla Sally Nyolo hajaingilia kati kwa-Tam Tam



Halafu ZAP MAMA amalizie tu tena kwa-Bandy Bandy


3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

emu-three 3:18 pm  

Mkuu umenikumbusha docta mmoja ambaye ni mtaalamu kweli kwa kazi yake lakini anabwia...tukajiuliza hivi huyu kasomea udocta na anajua amdhara ya kubwia???!

Goodman Manyanya Phiri 6:27 pm  

Ndio Mkuu, elimu haimbadili mtu kiini cha ubinadamu wake; na kama umezaliwa mpumbavu utaendelea na upumbavu wako pamoja na elimu yako ya juu. Vilevile kama umepewa busara ungali bado tumboni mwa mama yako, ndio hivyo tena pamoja na elimu ndogo ulienayo.


Mawazo yetu sote yanatawaliwa na utafutaji wa raha tu hata ukiwa dokta au kibaka.

malkiory matiya 6:57 pm  

Kazi ipo hapa, wapo madaktari walikumbwa na skendo za kubaka wagojwa zao,na wengine inasemekana bila kulamba ule unga wanautumia kwa anaesthesia operation haiwezi kwenda kama inavyotakiwa. Kwahiyo hapa tunaweza kusema ni kazi na dawa!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP