Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Neno likifikia KUMTAFSIRI MTU, huweza kufikia kumfanya MTU ajifananishe mpaka na neno limaanishalo SEHEMU za SIRI chafu!:-(

>> Thursday, July 14, 2011

Na neno kwa kuwa hufikia KUTAFSIRI watu,...

.... ndio maana ``MBWA WEE!´´ kuna wajijuao ni WATU bado huchukia,...
... kisa neno MBWA wanafikiri limemtafsiri MTU!:-(




Na neno likimtafsiri MTU,...
.... kuna wahitajio mpaka neno ``MHESHIMIWA´´ mbele ya majina yao kisa neno ``MHESHIMIWA´´´kwao kiheshima ndilo linatafsiri uheshimiwa wao kwa wafikiriavyo ndivyo wahitajivyo kuheshimiwa na WATU!:-(

Swali:
  • Si umestukia ukiachia NENO likutafsiri labda ndio unajenga mazingira ya NENo kuweza kukuathiri hata KIMATUSI?
  • Si unafahamu kuwa labda ni neno tu -na ukweli ni kwamba DUNIANI hakuna MTU mwenye KICHWA kama BOGA au titi kama embe bolibo-  kwa kuwa labda hayo NI MANENO TU?

Ndio,...
....NENO ni NENO tu na labda tatizo ni WATU wajifananishavyo na NENO kitu ambacho huweza kufanya MTU mwenye MENO kama NGIRI kujifananisha na NGIRI!:-(







Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!







Hebu Tshetsha Boys waanzishe tena kwa - Uya Kwihi Ka Rose



Au tu tupate tu na- Dikgomo remix

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

emu-three 11:25 am  

Watu husema akutakanaye hakuchagulii tusi...Jana kwenye daladala watu walipigana na ukiuliza kisa eti mmoja kamuita mwenzake `wewe mwanamke tu...'....je kuitwa hivyo ina maana kweli kama ulikuwa dume utakuwa jike...!

Simon Kitururu 4:04 pm  

Ndio hapooooooo!@M3

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP