Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

MWAJUMA kama akuteteaye ni RAFIKI ,chunguza TENA akuteteacho kwa kuwa labda kisemwacho na adui yako ZUBEDA kina mshiko !

>> Tuesday, July 12, 2011

Pamoja na mazuri yajayo na URAFIKI,...
.... moja ya udhaifu wa URAFIKI wawezakufanya MARAFIKI wamtetee MTU kwa sababu tu ni MARAFIKI zake,...
.... na labda ni ukweli kwa kugawa kidude HUYO ATETEWAYE na MARAFIKI sio kweli ana roho nzuri kisa sio mchoyo wamgao kama wadaiovyo MARAFIKI ,...
... kwa kuwa labda kuna ukweli labda uliopo ambao wausemao ndio wale MTU awaonao MAHATERS/MAADUI kisa mtazamo wao ni kuwa agawaye hovyo labda ni MALAYA huyo!:-(

Swali:
  • Si wajua kuna NDUGU na JAMAA/Marafiki ambao chochote ufanyacho wanajisikia kuwa wajibu wao ni kuwa upande wako hata kama labda unachemka?
  • Si yasemekana kuna WAAMINIO Utanzania moja ya maanayake ni KUTETEA Tanzania kwa kila kitu TANZANIA ifanyacho?


Ndio,...
....kuna uwezekano pia USHAURI mzuri na wakweli ,...
.... waweza kuwa ni ule UJIFUNZAO kutoka kwa wautoao wale UJUAO ni watakao KUKUANGAMIZA.:-(

Ni wazo tu hili MKUU!:-(


Hebu tukatizie Columbia ili Alfredo Linares aingilie kwa -Cachumbambe



Au twende New York .... Broadway ili tu tupate Fela Musical - Original Music kutoka kwa - Fela Kuti


2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

emu-three 3:28 pm  

Ndio mkuu, `lazima uwe mwenzetu ndio upate tenda...' au sio...lakini hata hawo wakubwa, wajionao ni wakubwa wa dunia, wanasema `ama uwe upande wetu-RAFIKI au wa maadui zetu..' ni hulka na udhaifu wa kibinadamu...UBINAFSI

Simon Kitururu 11:07 am  

Kweli M3 -UBINAFSI unanoma zake!:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP