DOGO ntakukalia uchi ULAANIKE wewe OOOHO- wee dharau tu WAKUBWA uone kilichomtoa NYOKA kwenye kishimo cha siri!!:-(
>> Thursday, July 07, 2011
Tukiacha na MKWALA huo hapo juu wa WAKUBWA ,....
... ambao labda ni wa kawaida katika maswala mpaka ya TISHATOTO,....
- Je unakumbuka KUHESHIMU wakubwa kwako MDAU?
Tatizo ni,....
.... kama kigezo cha UKUBWA sio UMRI,....
.....ukifuatilia ya WAKUBWA unaweza DHARAU aitwaye MKUBWA kisiasa ,...
.....hasa katika MAZINGIRA haya yetu ya SIKU HIZI ambayo UKUBWA sio UMRI na WAKUBWA bila hata aibu huweza KUTOJIHESHIMU kwa hata kufikia KUIBIA WANYONGE wawapao huo UHESHIMIWA.:-(
Swali:
- Kwani unafikiri ni kwanini siku hizi ``MHESHIMIWA´´ huwa ni neno lilazimishwalo kuwepo nyuma ya utambulisho wa waitwao WAHESHIMIWA hapa kwetu TANZANIA?
- Kwani unadhani UMHESHIMUYE Abdallah huwezi KUMHESHIMU tu bila kumuita MHESHIMIWA Abdallah kama swala ni HESHIMA?
Ndio,...
... kwa MIKWALA yadaiwa MKUBWA akikukalia uchi waweza kupofuka kilaana,...
... na kwa hiyo labda shukuru kama hujawahi bado kukaliwa uchi na WAKUBWA ukastukia NA KUJUA kitu ,.......kwa kuwa ukijua unaweza kujikuta umetukana MKUBWA kisa umejua undani wake na siri ya UKUBWA WAKE hata wa kiufisadi wa kodi za WAMACHINGA azitumiazo kumjengea KIMADA nyumba bila kusahau ufanyavyo kwa ambao bado hawajakaliwa uchi kuchukulia kuwa huo ndio UKUBWA ,...
.... kitu kiwezacho kukupatia laana ya KUFUNGWA jela au kuhakikishiwa HUPATI UBUNGE ili usije stukia zaidi kuwa labda LAANA za WAKUBWA labda ni MIKWALA tu kama UKUBWA wao wenyewe misingi yake hata bila kukaa uchi bado haina HESHIMA.:-(
Ni wazo tu hili MKUU!:-(
Hebu ghafla turudi BENIN ili Zeynab adinye - Bebe Yi Ga
Zeynab aongezee dozi kiuafrika kwa -Inan Ran
Au tu turudi TANZANIA ili Kassim atulize mshawasha kwa kudai - Usiende Kwa Mganga
Au sijui tu kwanini Kassim arudie tu na ile dozi - Awena
Kabla HUGH MASEKELA hajazima tena kwa-Afro Beat Blues
0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Post a Comment