Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

ENZI za:``Halafu nikaona BONGE la MIPAJA na udenda ukanitoka´´- ZIKIPITWA!

>> Saturday, July 02, 2011

Ladha na FASHENI ni kiboko,...

.... kwa kuwa yaweza kugeuza ATOKWAYE udenda LEO kwa kuona BONGE la PAJA,...
..... kubadilika LADHA kama PAJA kubwa likibadilika maana na kuashiria ULAFI/kula sana,...
..... au tu  kufanya MTOTO mzuri TIPWATIPWA kuonekana kanenepa hovyo  kama tairi la michelini,..
... na kwahiyo  kifasheni kama tu kiladha sio tena KIPOTABO na U-MISS MADABA hafai!:-(

Swali:

  • SI mwenye paja nono  UMISI kariakoo hapati sikuhizi TANZANIA kama tu  apendaye paja la kuku lililonona kwa wa MCHICHAMCHICHA/ MAVEJETARIANI huyo  anachemka kwa kuwa kitambi sio afya wala urembo kwao HASA kama hicho kitambi sio MIMBA?


Ndio,...
.... yasemekana enzi za BONGE la paja ni sifa kwa wazimiao VIPOTABO ,....
.....  hata kama kiongelewacho ni BONGE LA PAJA kiukiritimba wa serikali,...
......kwao hao KIBONGE mwenye bonge la paja kizembe  ANACHEMKA kwa kuwa hata kwa kiserikali ya vijiji  yasemekana UFANISI wa shughuli  HUYO  hawezi!:-(

Swali:
  • SI inasemekana ikizidi unono labda huo ni ushahidi haina AFYA?







Ni wazo tu hili lililopinda MHESHIMIWA!:-(

Hebu ghafla turudi BURUNDI ili Khadija Nin abadili kwa ndude-MAMA



Khadja Nin aweke kitu- Sina Mali, Sina Deni


Khadija Nin anyuke tena-Mwana wa MAMA



Khadja Nin amalizie tu kwa ndude iliyotuna-Leo Leya


4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Mija Shija Sayi 11:59 am  

Ndo hivyo, binadamu hatueleweki..

makala zangu 2:51 pm  

Simon Kitururu...umejaa mtandaoni na katika Mabloga wote wa Kibongo wewe si mchoyo hata kipenyo kuwajenga na kuwatangaza wenzio. Ingekuwa mabloga wote tuko kama wewe ukweli tungeendeleza sana Fasihi Simulizi,hasa Kiswahili, Afrika Mashariki!!! Unasindikiza na kuendeleza uandishi wa mtandaoni. Lugha nyepesi, Kiswahili kizuri cha chai, ulezi na maandazi.
Ila kitu kimoja nakuomba. Unachanganya sana rangi kimaandishi hadi saa nyingine inakuwa vigumu KUSOMA fikra zako nyoofu. Kaza uzi mwana kwetu!!!

Mwanasosholojia 5:35 pm  

"Mipaja" wingi (plural) ya "Mapaja" @Mtakatifu?..nawaza tu kama usemavyo..:-)

Simon Kitururu 7:46 am  

Da MIJA: Lakini kikueleweka labda TUNAELEWEKA ingawa labda ni kikibiongo!:-(

@MKUU Freddy MACHA:Asante kwa FUNZO na haki ya nani ASANTE kwa kunena kitu katika kijiwe changu na mie wewe tokea enzi ni moja ya shule ambayo mpaka nahisi labda ingehitaji nilipie ADA zaidi ya Kinyerere!:-(

@Papaa MITS: MIPAJA na MAPAJA: ni

MAPAJA labda kimipaja ,.
.... labda kuna MAKOVU!:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP