Tanzania NDOTO iko hai au NDIO imeshageuka JINAMIZI?
>> Friday, July 01, 2011
Kama ndoto ilikuwa ni kupata UHURU,...
.... baada ya UHURU,...
.... ndoto ihai au imeshageuka JINAMIZI?
Kama NDOTO ilikuwa ni kuwa na VIONGOZI wazalendo,...
.....ndoto ihai au ishageuka JINAMIZI?
Kama ndoto ilikuwa maisha bora kwa kila MTANZANIA,...
.... ndoto ihai au imeshageuka JINAMIZI?
Ndio,...
.....JINAMIZI ni ndoto BADO,....
... ila TANZANIA kama NDOTO ,...
... je ndoto hii sio JINAMIZI?Nawaza tu kwa SAUTI!:-(
Ijumaa na WIKIENDI NJEMA!Hebu tugawiwe Dream a Little Dream kutoka kwa- Louis Armstrong
The Golden Gate Quartet waingilie kati kwa - Nobody knows the trouble I've seen
Au hebu tubadili kwa kwenda tena Senegal ili Daara-J wakumbushie tena - Slavery
Halafu Konshens kwa kubadilisha wamalizie tu kwa - Insanity
2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Juzi mkuu tukiwa ndani ya daladala wengine tukiwa tunapaka rangi(tumesimama, hatuna siti)..kukawa na mjadala, wengi walikuwa wakisema kuwa ni heri tusingepata uhuru, tuendele kutawalia, kwani maendeleo yangekuwa makubwa...hutamini wanaoongea hivyo ni wasomi..
Hivi nini maana ya Uhuru? nikajiuliza kichwani na swali hilo likajibiwa hata kabla ya kuuliza kuwa uhuru ni hali ya kuwa na uwezo wa kujitegemea, na kutotawaliwa kwa aina yoyote ile...sasa je tuna uhuruu huo? ...mjadala ukawa mreefu, na ndipp nikawasikia hawo jamaaa wakisema ni heri tusingepata uhuru mapema kwasababau sasa ndio tunatawaliwa ile mbaya...kwa vipi nilishindwa kuelewa, kwani haiji akilini!
Hivi watu wanajua kutawaliwa kweli?mpo kwenu mnaambiwa msiendee choo hiki ni cha wadhungu, huku ni kwa bwana wakubwa, msitembelee mitaa hii kwasababu ni kwa wakubwa, msifanye hiki na kile kwasababu hamstahili...!
@Mkuu M3: Yani we acha tu! Inasikitisha sana ukifuatilia mambo yetu lakini!:-(
Post a Comment