Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

AKILI sio NYWELE na LABDA si kila mtu ANATUMIA zake!

>> Thursday, October 29, 2009

Na ni kawaida kukosea MATUMIZI ya akili,.....
....hasa kwa kuwa SIYE MTU KIBAO tunasahau kuwa ndani ya siku LABDA akili zetu hutumika zaidi SIO KWA KUBUNI na KUFANYA YA KWETU WENYEWE KIAKILI , bali kifanyikacho NI kutumia akili zetu ili kutumia yaliyoanzishwa na kufanywa na AKILI ZA WENGINE.

Na haki ya nani kuna WENGI tuishio bila kutatua yetu ya KIAKILI ZETU kwa kuwa zetu akili,....
.....zijuacho TU hata katika kuelewa ya KWETU, hakikamiliki bila kutumia akili za WENGINE.:-(

Kama unabisha:
  • Unafikiri kama wewe ni MKRISTO huhitaji kutumia yaliyokokotolewa na akili za YESU ili umwelewe YESU anamaanisha nini kwenye hata la kubatizwa ni kuzaliwa tena , au tu KWA UJUMLA UKRISTO WENYEWE hata kama huamini hii ANDUNJE NI kitu ambayo kwa kuwa INATEGEMEWA TAYARI KUNA AMBAYO HUTAELEWA, yabidi katika kukihalalisha KITENDO CHA KUWA MARA NYINGI KIDUCHU DINI HAZIELEWEKI, unaandaliwa uelewe yasiyoeleweka YA kufuata dini bila kuelewa KWA KUFUNZWA YASIYOELEWEKA KWA KUTUMIA AKILI ZA KIBINADAMU ni IMANI au yanaeleweka UKIWA NA IMANI TU?
  • Si ushawahi kusikia kwa imani utaponywa na kama imani yako mkweche hutapona HATA ukoma wa nanihii?

  • Na kama wewe ni MUISLAMU, unafikiri huazimi akili mpaka za SHEKHE ili tu uelewe utakacho kukielewa katika UISLAMU?
  • NA si unajua kama sasa hivi unatumia KOMPYUTA labda unatumia akili za wengine kama sio wewe uliyegundua KOMPYUTA?


Ok MKUU!

Labda kama kila mtu ana akili zake basi akili za watu ni OMBAOMBA kwa jinsi tu zilivyodoezi katika hata watatuayo idaiwao WANAAKILI inasahaulika labda walitatua kwa kudoea AKILI ZA WENGINE!:-(

WAZO nalikatizia hapa na UNARUHUSIWA KUNIBISHIA MUUNGWANA na katika SPIRITI ya kutokusahau KUTONIELEWA NI BOMBA LA Ruksa!






Au ngojea nikiri yamenishinda katika hoja hii kwa kusema...


Basi bwana mie ngojea nirudie kumsikiliza tena ASA akilalamika tena kuhusu-JAILER




Au tu Jimmy DluDLU arudishe tena JAZZ kutoka AFRICA.....

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP