Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

MAPUNGUFU ya swala zima la wapi KUNA MNUSO!

>> Thursday, October 08, 2009

Unaweza usistukie, LAKINI haitoshi kujua wapi kuna MNUSO,.....
.....kama pamoja na njaa HUJAMASTA staili zikuhakikishiazo hutaangalia tu bali utaweza pia KUKATA TONGE ili tumboni uende MNUSO!


Haki ya nani nakuambia ,BAADA ya kujua ulipo MNUSO,...
.... ni SAYANSI TOFAUTI kujulia staili ya KUUTOKEA na KUUBAMBA KUNAKO kama vile umekaribishwa vile kwenye huo MNUSO!:-(


Ndio maana ukichunguza wenye elimu watutishao kwa elimu kama tu waliostukia MNUSO,...
...waweza kushangaa elimu na vyeti BWELELE wanavyo lakini waweza kustukia wana KWASHAKOO kwa njaa pamoja na elimu kuwatoa TONGOTONGO na kuwastua ulipo mnusoLAKINI bila kuwapa pembejeo, mkakati au staili tu ya KUKATA TONGE ili mdomoni liingie na ILI ANGALAU tumboni utumbo uweze KUHARIRI sehemu zisizohitaji kugeuzwa mavi katika huo MNUSO.:-(
Swali:
  • Si unajua unaweza mpaka KUMJUA umpendaye KIPENZI lakini ushindwe kujua lakufanya angalau KIPENZI kama hataki kukupa yoteyote angalau akuazime basi angalau kidogo hata gizani ile kitu upendayo iliyomng'ang'ania KIPENZI?
  • SI unajua unaweza ishi kwenye maji mengi na kufa na kiu kwa kutojulia staili ya kuyachota maji kama tu yaliyoikumba bara tajiri lenye watu masikini liitwalo AFRIKA?


NIMEACHA WAZO Mkurugenzi!
Kumbuka hili ni WAZO TU Mheshimiwa !


Ngojea Jimi Hendrix abadili kwa kitu-Cross TOWN Traffic-



Au tu mwanadada SHEILA E atulize hali ya hewa kwa DRUM solo


AU tu tumuache tu aonyeshe maringo yake dingilidingili mpaka chini SHEILA E akiwa na TITO PUENTE...

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP