Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

PANUA ZAIDI KIDOGO basi mpenzi NIINGIZE!

>> Monday, October 26, 2009

[Tahadhari: Panuo katika hili wazo halina uhusiano na maungo.:-(]


MAPENZI ni kupanuliana,...
... kwa kuwa hasa kabla HUJAPANULIWA ndipo USTUKIAPO hata katika maisha YANAYOBANA ni KIBANO!:-(


NA katika PENZI hata liitwalo MAISHA kama wewe ni MUUNGWANA anayebana,....
...basi kama PENZI ni la KISWAHILI na hupanui wakati unakipanulio, KUNA uwezekano unalielewa PENZI kwa Kiitaliano na huelewi kwanini wengine PENZI = MAISHA na katika hilo labda HUHITAJI kujua KIRENO.:-(

Na ni kweli kwa apanuaye zaidi ajuacho huwa kinabana,......
......NI KWELI hupata zaidi MPAKA hata ujuzi wa ambavyo kwa kawaida INASEMEKANA hata malaya anabania, NA huyo NDIYE ASTUKIAYE mpaka kama WATANZANIA kabila ni WAPARE kuwa hata kwa WAPARE ili UELEWEKE wapo ambacho waongeacho KIPARE huitwa KIGWENO!:-(


NAACHA WAZO !
Kumbuka SI LAZIMA UELEWE kila kitu MAISHANI kama hata hiki HUELEWI, kwa kuwa KWA KAWAIDA kutoelewa ndio siri ya kuwa wewe NI BINADAMU!


Swali:
  • AU?

  • Si unajua UKIPANULIWA unaweza kuingiza au KUINGIA KIRAHISI ndio maana SI MAZINGAOMBWE mtoto wa KIKWETE ikiwa kirahisi kawa KIKWETE na mtoto wa MWALIMU NYERERE akashindwa kuwa NYERERE?
  • Unajua kunauwezekano kama umefanikisha kuna aliyekupanulia ingawa kijeba unataka tukusifie kuwa uliyofanikisha ni juhudi zako tu?

Hebu JIMI HENDRIX atoe dozi katika kitu kisicho mkao wa kitoto kigitaa....-THE SKY is CRYING



Au tu TINA TURNER akumbushie -BETTER be GOOD to ME


Au tu MwanaFA na LADY JAY DEE watulize boli KIBONGO kwa kitu-MSIACHE KUONGEA

5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

chib 3:50 pm  

Inabidi kunywa kwanza mwarobaini ili uelewe mada hii :-/

EDWIN NDAKI (EDO) 5:37 pm  

tutafika tu hata kama hatutaelewa..tunaweza japo tukalewa

Simon Kitururu 6:30 pm  

Jamani si akiriye kutoelewa kwa kawaida ndiye kuna kitu aelewaye ?

Fadhy Mtanga 7:22 pm  

Upo juu mkuu!
Katika siku zote leo ndiyo nimekusoma uzuri.

Lakini hiyo ndude ya Jide na Fa-msiache kunaniliu imesimama. Wenyewe kuchonga ngenga na roho za ngendembwe iwachome kiparanji.

Simon Kitururu 7:56 pm  

@Papaa Fadhy:Si utani NDUDE ya MwanaFA na JIDE imekaa kulia kweli ya kushoto.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP