Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

CHA AJABU ni kwamba, WENYE AKILI WENGI bado husomea ambavyo wangeweza KUVIJUA WENYEWE BILA KWENDA SHULE!:-(

>> Friday, October 30, 2009

Na ni kweli,...
...wengi wasifiwao kwa akili NI kwa sababu TU wanasomea ambayo kwao kirahisi wangeyajua tu bila MWALIMU!:-(

Na ni kweli,....
.... karibu kila mtu kuna kitu KWAKE ni rahisi kama KUNYA TU na wala si vigumu kama KIWASUMBUAVYO WENGI CHA kujulia jinsi ya KUTAWADHA VIZURI baada ya kuachia TIMBA , ingawa haki ya nani hata katika hilo la STAILI YA KUCHAMBA VIZURI wengi hufikia UGWIJI bila msaada wa MWALIMU!:-(

Swali:
  • Unabisha?
  • Kwani unataka kusema BADO hujastukia KUWA mpaka wenye vipaji vya asili vya kusukuma mkokoteni wapotezavyo muda kusomea kusukuma mkokoteni hata kama UDHAIFU wao uhitajio SHULE uko katika kumridhisha mama watoto na KWA HILO hata siku moja haistukiwi labda SHULE bora kwao ingekuwa ni ya kuridhisha mke na sio ile waahangaikayo nayo wakati hawaihitaji SANA ya kusukuma mkokoteni?

  • Kwani hujastukia kama MFUMO usingekuwa UNA VYETI vihakikishiavyo watu kuwa KIBONGE KAENDA SHULE kuna wengi wenye DIGIRII za VYUO VIKUU elimu yao katika swala ni BOMBA LA KINDEGATENI?

HILI NI wazo tu KISHTOBE na wala usitishike!
Ijumaa NA wikiendi njema MHESHIMIWA!

Hebu tupate tena ambacho kwa MAFISADI labda NI burudani kutoka TANZANIA kama iletwavyo na ile kitu -DARWIN's NIGHTMARE


Au tu hebu huyu Mbenini WALLY BADAROU atupe ile NDUDE roho ilipenda iitwayo - HI LIFE




Au tu Mkameruni BEBE MANGA amwage tena ndude roho ilipenda kwa jina-AMIO

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Anonymous 9:33 am  

simon,asante sana kwa kutuwekea miziki hii imenikumbusha mbali sana,yaani men asante ,i miss home!!!

Simon Kitururu 2:02 pm  

@Anony: Karibu Mkuu!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP