Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

KILA mtu ni MSHINDI ukibadili JAJI!

>> Thursday, October 15, 2009

Kila mtu na jicho lake,...
.....wakati kila BINADAMU na sikio lake.

Na ukibadili jaji, waweza kupata jaji mwenye jicho limdekulo KISURA sura kaa NYIGU kwa jicho ka LA mama YAKE limuonano Mzuuuri kama MCHUMBA wa MALAIKA!


Swali:
  • Unafikiri OBAMA kashafanya chakusababisha KATIKA WATU WOTE duniani yeye ndio awe Mshindi wa NOBEL PRIZE ya AMANI wakati ndio atoaeye sasa hivi amri watu wafe Afghanistani bila kuwepo dalili za amani ukibadili JAJI?


  • Si unakumbuka LAKINI kila toto udhanialo BAAYAA KAMA MIMI inadaiwa ni lizuri kwa mama yake?
  • Lakini kama toto baya KAMA MIMI ni zuri kwa mama yake wafikiri BABA LAKE TOTO HILO lipendwalo na mama huyo LIKOJE?

Basi MKUU hali halisi ndio HIYO,...
...kwa wengine SINDIMBA YAO ni BONGO FLEVA wakati wengine BONGO FLEVA YAO ni SINDIMBA na ukizidi kuchunguza utastukia mpaka kuna AMBAO kukoroma ndio sauti nyororo kwao.

Kwa hiyo kama umeshindwa ,KWA WENGINE wewe bado ni BOMBA la MSHINDI!
NI wazo tu Mwanakwetu,...
......ila kama WEWE ni mcheza Sindimba , kumbuka NA LEO umuhimu wa kuendelea kufanya mazoezi ya KUNENGUA , kwa sababu HALI HALISI yenyewe ya sindimba MJANJA ni YULE bingwa wa kukata KIUNO.:-(



NIMEACHA na usitishike, HILI ni wazo tu MHESHIMIWA!

Tupumzike kwa prank -Bride in the BUSHES


Au tu tujifunze kutoka kwa Nalts kuhusu jinsi ya kufanya video zako zipate watu wengi kama unamchezo wakuzipandisha kwenye YOUTUBE

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Fadhy Mtanga 10:27 am  

Hilo somo la kupandisha video katika YouTube ni babkubwa, ngoja nami nianze.
Nilipoteza mkuu, sasa nimerejea salama.

Simon Kitururu 10:19 am  

@Askofu Fadhy: Karibu tena!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP