Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Mie nailaumu BAOLOJIA, KEMISTRI na FIZIKIA YA MWILI kwa kun'tia DHAMBI!:-(

>> Tuesday, October 20, 2009

[Tahadhari: Wazo limepinda!:-(]

KIBAOLOJIA kunawatu ukipevuka inabidi uwatamani kama CHEMISTRI yako ya mwili inaendana vyema na FIZIKIA bila kuisahau ya mwili BAOLOJIA.

KIFIZIKIA niyatamaniyo KIBAOLOJIA na KICHWA JUU yanaweza kusahaulika kitamanicho kiko juu KWA KUWA ghafla labda nikitamanicho NATAMANI kukigusa chini na pembejeo ya chini na KUDHANI nakisikilizia kwa chini wakati kisikilizio hata ukionjea chini ni UBONGO uliopo juu KIBAOLOJIA.:-(

Na kisafirishacho utamu kwa NEVU a.k.a nerve za mwili ni kama umeme KIFIZIKIA,....
.....na kisababishacho mpaka niache kazi na kumendea KUTOKANA NA MAHOMONI chaweza kuelezewa na KEMISTRI za mwili, na hapa wala sitaki kugusia pembejeo iletayo ufanisi wa dhambi KIBAOLOJIA.

Kabla sijaendelea, SWALI kiduchu:
  • BADO wafikiri dhambi zangu ni kosa langu?
  • Unafikiri nisingekuwa na mwili ningekuwa na dhambi?

Ndio ina semekana kuna ya KISOSHOLOJIA yanayo KATALAIZI ya kisayansi yanifanye nifanye dhambi hata za KIBAOLOJIA.


Lakini ukweli uko palepale kuwa,...
.... kuna mambo kama wewe ni binadamu wahitajika kushusha damu KUNAKO CHINI kama wewe uko fiti KIBAOLOJIA,...
.... na kama hufanikishi hilo , labda unatatizo pia KIKEMISTRI na KIFIZIKIA na sio tu KIBAOLOJIA.

Na NI KWELI kuna michanganyo ya KIKEMISTRI na KIFIZIKIA ambayo ndio sababu ukichukizwa NI KWELI unachukia kikweli, halafu unaweza mpaka ukamwaga damu ya MTU na hapa naongelea kikumwaga MKONG'OTO na wala tena siongelei KIBAOLOJIA.

Halafu eti MASIKINI MIYE kwa udhaifu wangu wa KIUANADAMU nikitii BAOLOJIA , kemistri na FIZIKIA za mwili eti kuna MUNGU atanichoma kisa NA DHAMBI kwa kuwa nimetii hata nyege za chapati ambazo NAZO zinaletwa na SAYANSI ZA MWILI na kunifanya nikadokoa KITAFUNIO eti kwa kuwa sifuatilii maadili ya KISOSHOLOJIA!:-(

Nakatizia HAPA hili WAZO Banangenge MHESHIMIWA!

Swali:
  • Kama umestukia RADI inasafiri mwilini mwa mtu KIFIZIKIA, na kwa kula unalainisha chakula kwa makemikali KIKEMIA na unajua ukifa utaoza KIBAOLOJIA, bado huwezi kustukia kwanini FIZIKIA, KEMIA na FIZIKIA mwilini zanipa dhambi ingawa kijamii nalaumiwa na maadili mabaya KISOSHOLOJIA?

HEBU tu turudi Bongo Nyoso BINTI MACHOZI a.k.a LADY JAY DEE ft TID adai -Understanding




Au tu tuendelee kubaki AFRIKA Nneka atupe kitu-Africans

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

chib 6:29 pm  

Huo mtazamo wako.......
Mie naangalia kwa mtazamo wa kuwa ndio masomo yaliyonipa msingi wa kazi yang ya leo :-)

Simon Kitururu 6:34 pm  

@Mkuu CHIB: Mtazamo wako naukubali!

Lakini hizi baolojia, kemistri na Fizikia za mwili kweli hazitutii dhambi?

Bila Hormones kuna mahitaji tusingekuwa nayo na wala tu singekuwa tuna kitu KURIDHIKA tusingekuwa na hiyo KEMIA.
Bila Nerves tusingesikia utamu.

Na Bila baolojia fulani tusingetimiza dhambi!:-(

NI kwa mtazamo huo wa kushoto nimeapproach wazo hili!

Yasinta Ngonyani 6:52 pm  

Mmmhhh!Simon:-(

Simon Kitururu 9:23 am  

@Yasinta: Mmmmmh!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP