Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Sala ya LEO: Miungu MKIUMBA TENA WANADAMU , labda wajalieni nywele za KIZUNGU AKINADADA ZETU Waafrika !

>> Wednesday, October 28, 2009

NA tufumbe macho TUOMBE! NA kupiga magoti ni RUKSA .;


Kwa MIUNGU wahusika!

Naamini mmestukia kwa nguvu zote asilimia kubwa ya akina dada wa KIAFRIKA wakomavyo na KIPILIPILI.

Na naamini mnashuhudia mpaka AKINA KAKA wa KIAFRIKA nao walivyoshindwa kuwa msaada kwa kukosa WABUNIFU wa jinsi ya kulainisha nywele za akina DADA WAKIAFRIKA ili wasisumbuke na MAWIGI au tu katika kujiandaa MPENDEZO iwe rahisi kidogo ili wasilazimike KUIGA WAZUNGU , kwa angalau kuvumbua MASHINE zielewazo mpaka cha MUAFRIKA kipilipili.

Halafu na hawa akina KAKA nyie MIUNGU wafumbueni macho ili akina dada bonge la figa , TABIA nzuri PANA, akili ujazo TANI, MASHAVU ya KUMIMINA mwanana , Macho ya GOLOLI za nguti, SANGARA wamo, KUJAMBA pafyumu, wasipikuliwe katika kudakwa PENZI na wenye kalikiti mpaka kwenye masharubu ya KWAPA kwa kisa tu eti STAILI YAO ya nywele KIPILIPILI!


AMEN!

MNAWEZA KUFUMBUA MACHO SASA!

Swali:
  • Unauhakika kuwa ni kweli sababu kubwa ya asilimia kubwa ya Wasichana wa Kiafrika isemekanao wamefanikiwa kuwa na nywele zifanananazo na za Malkia Elizabeth ni kwakuwa tu ni vigumu kuhudumia NYWELE KIPILIPILI?

HILI NI wazo tu MHESHIMIWA na wala USITISHIKE !:-(

Ngojea Oliver N'goma na Bhonos wamsifie Mwanadada ambaye nahisi labda anakipilipili na twende kilioni imeanza kufumuka kwa mbaaaali aitwaye-Alphonsine



Au tu Oliver N'goma mwenyewe aendelee kumuongelea mwanadada mwingine kwa jina-Julie

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

chib 8:31 am  

Zamani akina dada walikuwa wanatumia chanuo la chuma lilikokwa kwenye moto na kutengeneza nwele za singa. Kuna wachache walikuwa wanaungua. Baada ya kuja hizi za bandia ....
Kumbuka na wazungu sasa hivi baadhi yao wanabadili ngozi zao waonekane weusiweusi vile..

Simon Kitururu 1:38 pm  

@Mkuu CHIB:

Hii inaonyesha kuwa kama tu tekinologia ya viatu vya Mchaga kajitahidi tulivyoachia katikati kuiendeleza ingawa tulikuwa na SIDO , ili tupate viatu vyetu kivyetu na PIA tekinolojia ya kurahisisha uandaaji wa ulimbwende wa nywele za KIAFRIKA nayo ikaishia kwenye chanuo la chuma lililokaangwa.:-(

Ingekuwa bomba kama kuna mtu atakayegundua vimashine vidogovidogo ambavyo kumsuka mabutu mdada dakika moja,staili ya Twende kilioni dakika moja na nusu,Staili ya nywele ya namtamani mme wako dakika mbili,....nk. labda ingesaidia kitu katika mionekano ya akinadada Waafrika waonekane Waafrika kama nia yao ndio hiyo lakini.


Nahisi na hawa Wazungu uliowataja itabidi niwakumbuke kwenye sala ijayo kwa Miungu!:-)

Fadhy Mtanga 6:48 pm  

Duh! Mi niseme nini wakati ni moja wa wategwao na nywele 'artificial'?

Simon Kitururu 3:23 am  

@Papaa Fadhy: :-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP