Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

JINSI ilivyokuwa kuna uwezekano MAISHA ya MTU AYAISHIO yanafuata mitazamo ya WATU WENGINE!

>> Wednesday, October 14, 2009

LABDA kuanzia UVAAVYO,...
....''YANI JAMANI!''

[Samahani!Sentensi ''YANI JAMANI'' inasikika kwa MTAMKWO wa huruma wa mwanadada KIBONGE mpoleee!:-(]
.........imetokana na unavyofikiria jinsi wafikiravyo WAKUTAZAMAO wengine!:-(


Bila kusahau LABDA hata UTEMBEAVYO,...
....''YANI JAMAANI!''
[Samahani!Sasa hivi hii sentensi''YANI JAMAANI inasikika kama vile imebaniwa pua na mdada mwenye mafua kwa mbaaali!-(]

... .........mwendo wako wa kujizuia kutikisa tako NI kwa kuogopa watakavyofikiria wakupigiao shingo hao WENGINE.:-(

Kwa bahati mbaya labda mpaka MAISHA baada ya KUFA a.k.a KUDEDI uyafikiriavyo,...
...labda umefunzwa tu mpaka KUTISHIKA ambayo ndio sababu unapiga SALA TANI wakati labda SALA UZITO DEBE ingetosha kwa kuwa tu kuna uwasikilizao na kuamini KWELI YAO hao wengine!:-(

Kwa kifupi nachojaribu kusema swala hili na najua unajua sijui HASWA ulivyo,...
....LABDA kusingekuwa na WENGINE wewe ungekuwa BOMBA la mtu MWINGINE!:-(

Kumbuka tu kuwa pamoja na yote AKUJUAYE VIZURI ni wewe mwenyewe na wala sio watu wengine.

NI wazo tu KINGUNGE na wala usitishike!
Swali:
  • AU?
  • Hujastukia uwezekano wa kuwa angalau BAFUNI wewe bingwa kweli wakuimba hata KICHINA kama hakuna watu wengine?
  • Kwa mtazamo fulani si kuna uwezekano mpaka wafuatao dini fulani wangefuata dini nyingine fulani kama wasinge fuata mitazamo fulani waliyoikuta kwenye familia zao ya watu wengine?
BASI NIMEACHA MUUNGWANA!

Ngojea BIDA atukumbushe kuhusu-URAFIKI WA UTATA


Au nimuache MAD ICE aendeleze katika MEDLEY ya songi TATU (Live)Rose, SHAKE na You Follow me

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP