Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Mtu mmoja NI WATU ELFU, na mpenzi siku ya kwanza SI YULE YULE TENA kuanzia siku ya pili NA baada ya miaka!:-(

>> Friday, October 02, 2009

Mpenzi siku ya kwanza,...
.....inawezekana mpaka sababu unafikiri anarembua ikawa ni kwa kuwa anakuonea tu AIBU.



Na mpenzi kwa MADAIRO mara ya kwanza,...
.... pamoja na kwa kwakukuficha ZAIDI YA upaja kavaa baibui , kwa hamu anachokitaka aweza kivalia UBUBU.



Mpenzi siku ya kwanza,...
... awezadai hata kula hasikii njaa eti kwakuwa mpenziye yu KARIBU.



Na mpenzi kwa kumsogelea mara ya kwanza,.....
..... moyo wake wawezakimbia riadha mpaka mrindimo wa mapigo UKAHARIBU.




LAKINI mpenzi baada ya MIAKA,...
.... akiwashwa sehemu za siri AWEZA kutaka UGEUKE NESI na umchungulie kunako NANIHII na kama kuna kipele ukibinye ukikitolea macho kwa KARIBU.




Na ukiendelea kumchunguza mpenzi baada ya MIAKA,.....
..... mpenzi ashakuwa ni mwingine na si yule UKIYEMUWANIA kisimani KWANZA na labda HATA hanukii TENA kama vile kwanza kwa KARIBU.



Ukiwa na mpenzi NI mwanaharamu kweli MIAKA,...
..... kwa kuwa ghafla penzi lageuka mazoea na labda hata chupi iliyotoboka hasiti KUENDELEA kuivaa na kujamba mbele zako si tena tendo la AIBU.



Lakini hongera kama lako penzi lishadumu MIAKA,...
.... kwa kuwa hata wewe sio yule uliyekuwa kwanza na siri yako na yake mpenzi ,labda kwetu ingawa bado sio CHA BANIANI KIATU na kwahiyo SI msaada lakini yaonyesha kwenu ni gundi ya uhusiano kama si dawa na TIBABU!


Swali:
  • Unafikiri wewe wa jana ni wewe wa leo?
  • Unafikiri KABLA hujamzoea mtu na BAADA ya kumzoea mtu, wewe unabakia ni YULEYULE vilevile?
  • Unakumbuka ukilizoea kanisa lenye mahubiri makali ya kutisha laweza geuka cha kutongozea kiwanja?

NI WAZO TU MHESHIMIWA na USITISHIKE!
Na nakutakia Ijumaa na Wikiendi njema MKUU!



AU Ngojea CNN basi wabadili kwa kutujulisha -WHY women have sex



Au ngojea N.W.A wabadili zaidi kwa kitu-Express Yourself



Au to KRS1 amalizie kwa kukumbushia enzi za -Sound of da POLICE

5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Faith S Hilary 3:09 am  

Ukimzoea mtu unakuwa kama kwenye "comfort zone" ambapo unafanya chochote kile bila kujisemeza kitam-affect vipi huyo mtu mwingine, naona kama ni nature ya mwanadamu na feelings zake...

Mwanasosholojia 10:34 am  

Mhh!Kaka, umenigusa ile mbaya..mambo ya leo si kama ya jana...ulimi ukizoea utamu huanza kuhisi kawaida..Heko!

Yasinta Ngonyani 3:22 pm  

Aibu sijui maana yake nini:-(

Markus Mpangala. 5:09 pm  

NIMETISHIKA MHESHIMIWA! lakini hata puto laweza kuwa bora mara unuapo...badae likapunguza nguvu na kuwa laini lenye kila dalili za kupasuka. Pengine kugundua kuwa jana siyo leo au kusahahu kuwa kula sana unaweza kuvimbiwa......

CHA AJABU kwakuwa kuna njaa leo basi tunasahau uvimbiwaji wa jana. HEKAYA TAMU hizi.....
Mkuu! nikusalimie kwa mchezo wa kombolela. Tyari au bado?

Christian Bwaya 5:24 pm  

Mkurugenzi nimepita kupunga mkono tu...

Tuko sote!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP