MIAKA 60 ya CHINA , Ubepari korokocho na UKOMUNISTI OYEEEH!
>> Thursday, October 01, 2009
Unaweza kukataa!
Lakini ukweli uko palepale kuwa BAADA ya miaka 60 ya ukomunisti na chama kimoja, CHINA leo hii ndio inaongoza kwa ukuaji wa uchumi DUNIANI.
NA tunaweza tukabobea kwenye mapungufu ya CHINA kama yahusuyo HAKI za BINADAMU, mazingira, na mengine kemkem. Au tunaweza hata kuzungumzia jinsi CHINA na ukomunisti wake inavyotegemea nchi za Kibepari katika ukuwaji wake kiuchumi na hata kisayansi na tekinolojia. Na labda kuna sababu nyingi NYINGINE zionyeshazo China itabadilika na kuwa nchi ya vyama vingi baada ya miaka kadhaa na jinsi kidogo kidogo inazidi kuendesha uchumi kibepari ingawa bado inatawalwa Kikomunisti kama dalili kuwa baada ya miaka kadhaa itageuka kuwa FULU UBEPARI.
.....ILA KITU kimoja lazima tukubali, ....
.....WACHINA wamefanikiwa kuigeuza nchi yao kivyao. Na mpaka sasa hivi bisha usibishe staili yao kivyao inalipa. Na leo hii ni vigumu kumkuta Mchina hata ambaye anapinga Ukomunisti na jinsi iongozwavyo china asiyejivunia ilipofikia CHINA leo.

SWali:
- Unafikiri Tanzania tunatatua matatizo yetu Kitanzania ikiwa hata Kiswahili tunataka kufuta mashuleni?
- Hivi hata SIDO ipo tena BONGO na unafikiri ilimsaidia nini fundi viatu a.k.a Mchaga kajitahidi wakati mambo zake yalikuwa kila mkoa fulu kuonekana?
- Unauhakika unajivunia Tanzania tukiachia mbali KILE kila Mtanzania aimbacho AKITEKENYWA TU kuwa tuna AMANI ingawa ubwabwa hautoshi?
KUDADEKI ni HILO TU!
Hebu tuideku TZ a.k.a BONGO NYOSO
3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Kama kawaida yako, umegusia jambo la msingi sana. Historia inatuonyesha kwamba jamii zilizoweza kupiga hatua "kimaendeleo" ni zile ambazo zilifanya utundu zikajinasua kutoka katika mduara tegemezi uso fundo na kuchagua njia na falsafa zake zenyewe. Wachina ni mfano mzuri kabisa. Sisi tunajaribu kuiga na sasa hata Kiswahili - lugha ambayo ipo tayari kutufanyia kila kitu tunaipiga dafrau na kuingiza lugha ya "walioendelea" Kazi bure!
Wachina wapo juu mbaya.
@Profesa: Yani inasikitisha!
@Askofu Fadhy:Si utani na kwa ujanja eti wanatuuzia mpaka dawa za kukuzia makalio ya dada zetu!:-(
Post a Comment