Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kwa kuwa bado Bin-ADAMU anastukia nani dumeJIKE !

>> Wednesday, October 21, 2009

Kwa kuwa tabia ni TABIA ,...
.... basi ni kweli tabia zenyewe hazina UUME au UKE!

Na ni tafsiri tu za tabia,...
..... zifanyazo watu wafikiri ni za KIUME au KIKE.


Mazoea mwanaharamu kweli kwenye tabia,....
.... ndio maana dume zima likitingisha kalio katika kutembea, ingawa mwendo hauna jinsia kuna watakaoapia lina mwendo wa KIKE.

Na mpaka shughuli tu zenyewe na si tabia,....
...... kuna wamuonao mwanamke hafai kuzifanya kwa kudai sio za KIKE.


Na kuhusu shughuli na tabia,...

....kirahisi wawezakuta ni RUKSA katika jamii fulani mwanamke kuwa NGANGARI shambani na nyumbani(hasa kwa watoto) na aonekane bonge la MAMA WATOTO , lakini mwanamke NGANGARI ofisini kirahisi aonekana analeta kibezi cha kiume na si mahali pake kwa kuwa yeye MAWANAMKE.:-(

Ngojea nilikatishe denge wazo:

Nacho jaribu kukokotoa hapa ni kuwa , kama jamii inastukia dumeJIKE,....
.... basi jamii inamtazamo wa KATIKA JINSIA nini ni SAWA na ni nini si SAWASAWA.

Na kama jamii inamtazamo ni nini cha kiume na nini ni cha KIKE,...
...... ni rahisi kwa jamii kuchanganya ni nini kati ya WANAWAKE na WANAUME ni muhimu kuwa sawa na ni nini ni baraka kuachwa viwe sio SAWASAWA.

Na kama HUJASTUKIA hasa katika maswala ya usawa wa WANAUME na WANAWAKE,....
..... kirahisi kuna watakao kila kitu , NA NAMAAANISHA kila kitu kiwe SAWA.

Na labda wakati unapigania usawa kati ya WANAUME na WANAWAKE,....
....kumbuka tu pia ni BOMBA la aidia kuwa BINADAMU WOTE NI SAWA kama ukikumbuka ukweli pia BINADAMU WOTE NI SAWA lakini SI SAWASAWA.

Swali:
  • Katika kupigania haki za binadamu unafikiri maana yake ni kufuta MWANAUME kuwa MWANAUME na MWANAMKE kuwa MWANAMKE?
  • Labda ni haki yako DUME zima kutaka nawe uwe na bonge la TITI, lakini bado si kuna starehe wanawake wakiwa na tabia za kike na wanaume wakiwa na tabia za kiume?
  • Umeshastukia dunia inaingia katika kipindi ambacho kirahisi unaweza usistukie ni nini tabia za KIUME au ni zipi zile za KIKE?

AU ngojea niseme:

NAKUWE na HAKI za binadamu kwa wote,.....
...... lakini tusichanganye kuwa hata kibaolojia MWANAUME ana uume na MWANAMKE ana UKE kwa hiyo KIUBINADAMU TUKO SAWA lakini vile vile hatuko SAWASAWA ambacho sio lazima kuwa ni TATIZO na kusema ukweli ndicho kiletacho starehe ya UNYUMBA.


Na ni vigumu kila mtu kujaribu kuwa yote,....
...... kwa kuwa KILA MTU ana ubingwa eneo lake na ni UTAMBUZI wa HILO ndio uletao ufanisi wa yafanikishwayo na MWANAMKE na MWANAUME wakiwa kwenye UNYUMBA.

NA wakati tunapigania haki za wanaume au wanawake katika yote,....
..... tukumbuke tu kuwa ni haki ya kila mtu kufanya yote awezayo lakini tutii pia kuwa MWANAMKE na MWANAUME tofauti zipo pia na zinajulikana hata KUNYUMBA.

NA tukumbuke tu WAKEREKETWA wa HAKI ZA BINADAMU kuwa si wakati wote,.....
..... ni vibaya kutambua kuna mambo ni WANAWAKE wamebarikiwa zaidi hata kuyastukia na si msuli tu wa kiume wenye suluhisho wa ya KUNYUMBA!

Na kwa kutambua tofauti zipo hata kama si kote,....
.....vita za haki za dume JIKE nazo zaweza eleweka ofisini mpaka KUNYUMBA.
Swali:
  • AU?

DUH NAACHA kwa maana topiki KUBWA na IMENISHINDA!:-(





Hebu Hugh Masekela ABADILI HALI YA HEWA akiwa na Paul Simon waje live


Au tu Miriam Makeba akiwa na Paul Simon waje nao live...

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP