Saturday, October 31, 2009

Wakati karibu kila mtu ANAJUA kuwa NIPE KIDOGO NICHANGAMSHE DAMU kwa kawaida hugeuka ''NIPE YOTEYOTE, yote tu JAMANI!'':-(

[Tahadhari: Katika kichwa cha habari sentensi ''NIPE YOTEYOTE, yote tu JAMANI!'' imebaniwa pua na Limdada zuuuri!:-(]


KIDOGO ni chachandu,....
.... na ikizidi kwa kawaida utavimbiwa.:-(


KIDOGO ni utundu,....
..... ikizidi maana yake huweza kutafsirika kuwa umeharibikiwa.:-(


Na kijuacho ukubwa kwa kawaida KAMA ni tundu,....
....basi kwa hilo si lazima mpaka tundu liwe KUINGIZWA limejaribiwa.:-(

Ila kwa kuwa Binadamu ni watundu,...
....DUNIA INAHARIBIKA SASA HIVI kwa kuwa TU mpaka binadamu wakijuacho kidogo wanakitaka kwa ukubwa na MAKUBWA YOTE KILAFI , na ndio maana wanaonja mpaka VYENYE SUMU VILIVYO tayari JARIBIWA.:-(

NALIKATIZIA HILI WAZO HAPA na unaruhusiwa kuliendeleza KIVYAKO MHESHIMIWA!:-(
Lakini swali KIDUCHU:

  • Unafikiri si kweli kuwa WALIOONJA KIDOGO na kujua ni tamu kwa kawaida hutaka makubwa yote ingawa wanajua kuwa hata asali ingawa tamu kuinywa, KUNYWA LITA kwa kawaida ni tofauti na kuilamba asali kidogo katika ujazo na KWALITI wa uupendao utamu?
  • SI unajua siri ya kilele cha utamu hupatikana kwa kuonja kidogo tu?
NIMEACHA na kumbuka hili ni wazo tu!
KUMBUKA PIA kuwa KIJIWE HIKI cha MTAKATIFU Simon Kitururu sio YESU wala NYERERE kikukorokochoa!:-(


JUMAMOSI NJEMA Mheshimiwa OTHRONG'ONG'O!


Hebu basi tusukutue uchafu wa wazo kwa kumsikiliza M-Ivory Coast mdada Monique Seka akilainisha kwa ndude iitwayo-Okaman

Au tubaki naye tu Monique Seka afanye matusi katika kitu -Missounwa

4 kommenttia:

Yasinta Ngonyani said...

Jumamosi njema nawe pia kaka Simon:-)asante kwa muziki

SIMON KITURURU said...

@Yasinta: Asante sana wewe pia kwa kutochoka kunitembelea!

Fadhy Mtanga said...

Muziki wa huyo mdada huwa UNANIKUNA hadi najishtukia NIMEZIDIWA na UTAMU hadi huwa natamani YOTEYOTE maana nafsi INAKONGEKA kwa staili ile ile ya ukipata kidogo UNATAMANI kuitumia YOTE na ikiwezekana iwe mali YAKO wewe peke yako bila KUINGILIWA na MTU.

Pamoja sana mkuu Mtakatifu Simon Kitururu a.k.a mzee wa kunogewa hadi kutaka yoteyote.!

SIMON KITURURU said...

@Papaa Fadhy: :-)