Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

WASUKUMA/Watanzania - The Dannish Saga

>> Sunday, November 01, 2009

Moja ya kitu kilichonisikitisha wiki hii kuhusu Watanzania,...
.... kina uhusiano na MTANZANIA aliyeua mke DENMARK.

Kama hujui kisa hiki unaweza kukifuatilia katika website ya TANDEN HAPA



Ingawa tukio zima ni la KUSIKITISHA, kitishacho ni kustukia baada ya kutembelea websites na CHAT ROOMS kadhaa kuwa kuna WATANZANIA ambao kirahisi KUKITOKEA MATATIZO huwageuka Watanzania wenzao kwa misingi ya kikabila.


Nimekutana na kuchat na watu ambao wamegeuza tatizo la Mtanzania huyu kuua MKE kuwa ni tatizo la Wasukuma. Nashangaa Watanzania ambao kirahisi hupenda kujishebedua kuwa Watanzania si wakabila WATANZANIA TUKISIFIWA KWA HILO , kirahisi kutenga watu kwa kufikiri mpaka jamaa ni kabila gani.:-(

Utashangaa kisa hiki kuwa kuna watu wanakitumia kuhalalisha kuwa kuna makabila ni wauaji kiasili kwa kuwa eti kuna ripoti za maalibino na vibibi vizee kuuawa mitaaa ya kwao.Na kitishalo kwa hilo ni jinsi ionyeshavyo watu waaminivyo sana msemo samaki mmoja akioza basi wote wameoza.:-( Na kwa mtazamo huo potofu naamini ukiachiwa utambulike kuwa ndio kweli yenyewe, BASI naamini kujikwamua kwa Tanzania na Watanzania kutabakia kuwa ALINACHA TU.

JAMANI tukumbuke tu kuwa UKABILA UPO SANA Tanzania na unawezashangaa ujitokezapo ,na kama wewe ni MTANZANIA USIJISAHAU kuwa pamoja na kupenda kabila lako basindio iwe ni misingi ya kudharau MAKABILA YA WENGINE.

Mimi naamini UKABILA si kitu kiwezacho kuwa msaada kwa Tanzania na kwa WATANZANIA sasa hivi!

Na JAMANI kumbukeni kuwa hakuna kitu kizuri kama umoja hasa wakati wa matatizo ingawa imezoeleka tu kuonyesha umoja WAKATI MAMBO NI SHWARI!


Na katika tukio hili la kuua mtu, tukumbuke kuwa tatizo sio USUKUMA au UTANZANIA kama unazingatia kuwa hili jambo ni binafsi. Na mambo binafsi ya kifamilia mtu wa nje kuyaelewa ni vigumu kwa kuwa KAMA WEWE sio MHUSIKA na huyaishi maisha ya mhusika, kumbuka UELEWAJI WAKO WA KITU UNAATHIRIWA na UDHAIFU wa kuwa unajaji kitu cha mwingine kwa kutumia uzoefu wa maisha yako ambayo hayafanani na unayemjaji MHUSIKA.

NI MTAZAMO TU WANGU katika swala baada ya kukerwa na UKABILA ULIOJITOKEZA katika kumjaji huyu MBONGO aliye.........:-(

Mungu amlaze pema MAREHEMU !
Mungu ibariki Tanzania!


Mie ngojea niendeelee kumsikiliza Warren G katika -Regulate


Au tu Warren G arudie tu -So many ways

6 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

nyahbingi worrior. 12:22 pm  

mkuu Simon,nimekupata.

amani.

Yasinta Ngonyani 1:38 pm  

Ni kweli inasikitisha sana kufa kwa namna hiyo. marehemu astarehe kwa amani

Faith S Hilary 3:30 pm  

Nimelipenda wazo hili, yaani nimezimikia kabisa. Wote wangekuwa wa-Danish who would mind? It's a murder case just as any other murder cases!

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) 6:35 pm  

Bwana Simon - ukabila, udini, chuki na uhasama upo na umeibuka kwa nguvu sana hivi karibuni. Naamini hii ndiyo sababu iliyoifanya ZE UTAMU iwe maarufu sana (soma hapa: http://matondo.blogspot.com/2009/06/ati-ze-utamu-imetufundisha-nini.html)

Sasa leo baada ya kufikiri jinsi ya kumsaidia huyu Mtanzania au familia na watoto wa Marehemu, watu wanaanza kushambulia Usukuma wa muuaji. Usukuma wake una uhusiano gani na mauaji aliyoyafanya? Muuaji angekuwa Mchaga, Mnyakyusa, Mhaya, Mkurya, Mpare au kabila jingine pia kabila lake lingeshambuliwa? Au kuna chuki spesheli dhidi ya Wasukuma?

Na hii ni Tanzania ambayo muda mfupi tu uliopita ilikuwa na kiongozi ambaye alijitahidi sana kuhakikisha kwamba udini na ukabila unapigwa vita kwa hali na mali. Mimi sijui tunakoelekea!

Simon Kitururu 7:44 pm  

@Wote: Yani inasikitisha!:-(

chib 10:56 pm  

Nimeupenda msimamo wako Kitururu.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP