USIONJE - ukinogewa NA DHAMBI kabla YA kuizoea JE?
>> Friday, November 13, 2009
Kuna uwezekano KUONJA ndio chanzo cha KUNOGEWA na KITU,......
..... INGAWA kumbuka,....
....ili mtu azoee KITU kwa kawaida INABIDI kuwe na WINGI WA HICHO KITU ,....
....na HAKI YA NANI TENA wala labda sio kweli MAZOEA HATA YA KUNOGEWA KIDUDE au KITU ni kwa sababu ni kitamu KIDUDE au HICHO KITU kama tutachunguza wingi wa matumizi yako ya KIDUDE au hicho KITU.
Swali:
- Unauhakika ugali ni mtamu au ni mazoea tu YA UGALI yafanyayo ufikiri si maharage ulayo na ugali yasababishayo uzoee kunogewa na ugali ambao kwenu BONGE LA UGALI KWA WINGI ni dozi kwa siku mara tatu?
- Unafikiri bila kuonja - hasa kama wewe ni miongoni mwa waoga kuonja- utakuwa na uhakika ungeonja ungenogewa na kuzoea kweli kitu?
- Si inasemekana ikibidi unaweza jikuta umezoea hata kuchambia mchanga kama maji, jiwe , majanijani , randi zilizoanza kubanduka katika ukuta wa choo, na tishu mchangani uendako kuchimba dawa havipo na wala havikuwahi kukunogea?
NI WAZO tu hili MHESHIMIWA!
Kwa mara nyingine SHIKAMOO basi na IJUMAA na WIKIENDI NJEMA ,nikisisitizia KAMA UTACHEZANAYE ukumbuke kucheza kwa STEPU na USIMKANYAGE MWENZIO!
Kwa mara nyingine SHIKAMOO basi na IJUMAA na WIKIENDI NJEMA ,nikisisitizia KAMA UTACHEZANAYE ukumbuke kucheza kwa STEPU na USIMKANYAGE MWENZIO!
Hebu Labi Siffre arudishe-Watch ME
Au tu AWILO LONGOMBA aanzishe ijumaa na kitu -MONDONGO
10 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Hapo kaka itabidi uombe radhi kwa wasukuma na wakurya hasa kipengele cha 'ugali'.....lol
vinginevo tutakupa likizo kama Zito....lol
@Kadinali CHACHA aka Ngwanambiti: Samahani kwa Wasukuma na Wakurya!
Lakini hivi ugali wa Wasukuma kwa Wakurya ni Mtamu?
tena sana...lol
hapo tena usipime...lol
Tena unapikwa mkubwa kinoma ambao hamuonani mpaka mnaulizana 'ng'wana-masangu, uli-he?'.....lol
Yaani mtoto wa masangu....uko wapi?...lol
Mmmmhhh hapa kazi ipo kaka Simon imechokoza nyuki:-(
Mkuu... hapo umezidi, nani alikuambia rangi zinazobanduka chooni unaweza kuzichambia?!!! :-)
@Kadinali Chacha a.k.a Ng'wanambiti & Da Yasinta: :-)
@Mkuu CHIB:Enzi za boarding school nilistuliwa ni kwanini rangi chooni zinabanduliwa hasa magazeti ya kuchambia yakiadimika.:-(
Chacha tehe tehe tehe..................
@kitururu, Chamba tu
Mie mgeni hapa. umesahau magunzi! nani hajawahi kutumia gunzi ajitokeze hapa.
hivi mazoea ni kwa vitu vizuri tu. hivi mmewahi kusikia mtu aliyepelekwa kwenye raha akidai kurudishwa kwenye shida eti hajazoea raha bali amezoea shida?
We Mwaipopo :-), mie nafikiri hiyo ya magunzi ni staili ya nyanda za juu kusini.
Watu wa sehemu za majabali sisemi ni wapi, lakini wao wanajua kuserereka kwenye mawe baada ya kutoa volkeno mbaya
@ Wote: :-)
Post a Comment