Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

NISIFIE nianze KUHARIBU!

>> Wednesday, November 25, 2009

Kuna waharibuo baada ya KUSIFIWA,...
.... kwa kuwa BAADA YA KUPATA SIFA wanapandisha mdadi wakuongezea MANJONJO,....

... bila kusahau kuwa kuna WAHARIBUO baada ya KUSIFIWA kwa kuwa wanaanza kufikiria SIFA WASIFIWAZO zaidi na kuacha KUFANYA tena KILE KILICHOWAPA sifa.:-(

Swali:
  • SI unakumbuka kuwa duniani kuna sifa za uongo?
  • Si labda unakumbuka jinsi wewe mwenyewe ulivyobingwa kila upatapo chansi ya kusifia watu ujuayo ni UONGO?


Tukiachana na hilo:

Inasemekana SIFA,....
....... ukimsifia hata MTOTO - mtoto anaweza akajitahidi zaidi katika USIFIALO.

CHAKUSIKITISHA kuhusu SIFA,...
...sifa kama tu yalivyo MAISHA MAGUMU, - sio CHANGAMOTO kwa kila MTU ili AJITAHIDI vizuri katika LIMKABILILO.


Nachojaribu kusema ni:

WATU tunatofautiana na katika hilo KUNA AMBAO ili WAJITUME huhitaji sio kusifiwa, - bali ni KUFINYWA!:-(


Swali:
  • Si unajua kuna watu AMBAO ni MAISHA MAGUMU ambayo ndio siri ya kujituma na mpaka ya MAFANIKIO YAO na kuna watu wengine ambao MAISHA MAGUMU HAYOHAYO ndio sababu wanampango wa KUJIUA?

  • Hujawahishuhudia MWANAFUNZI aliyesifiwa na kuanza kudharau Mwalimu kwa kuwa anafikiri bila ushahidi kuwa kakubuhu kwa kujua kuliko MWALIMU?


Ngojea AVANT ashauri-Lie about US

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) 6:14 pm  

Mgema akisifiwa.....

Simon Kitururu 3:58 pm  

@Profesa: Mgema akisifiwa anafikiria azidishe ujazo wa kinjwaji bila kinjwaji.:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP