Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

UKITONGOZWA UKAKUBALI!

>> Tuesday, November 03, 2009

Duniani hakuna ambaye hajawahi KUKUBALI,....
.... na inasemekana mtu aliyekubali kinamna huyo KABADILIKA tokea tu akubali!

Mimi naamini kilichopo ndani ya aliyekubali,....
......kilikuwepo tokea hajapewa ombi na akakubali.

Swali:

  • Unafikiria ni maisha yako au wewe mwenyewe unayebadilika baada ya kukubali mtongozo?


Labda,...
...UKITONGOZWA UKAKUBALI kilichobadilika sana ni hicho tu kuwa UNAJIJUA ulitongozwa UKAKUBALI,....
.....hata kama siye wengine HATUJUI NANI MAISHANI UMEWAKUBALIA kwa kuwa ukweli wenyewe wewe mwenyewe uko vilevile MGUMUUUU kukubali.

Kukubali kunaweza kukuua uhuru,....
..... ingawa pia kwaweza kwenye mwanga kukutoa NURU.

Lakini kumbuka hata kwa idaiwaye kabadilika kwa kuwa baada ya kutongozwa akakubali sikuhizi anakukuru,....
..... kumbuka aliyeshwari anakukuru PIA ukimpa kiwanja na sababu ya kuonyesha zake kukuru.

Na INAWEZEKANA kila mtu ana mpaka umalaya ndani yake akijipa uhuru,....
.... na si kweli limtu malaya hujifunza tu umalaya kutokea zero wakati linataka kuwa malaya NA HALIKUWA NA CHEMBECHEMBE ZA WAZO LA KUGAWA KIRAHISI LIKICHEKEWA TU tokea bado LINAFIKIRIA KILOKOLE , kama ukichunguza ubongo wa binadamu ufanyavyo kazi na kwa hilo ukapata NURU.:-(


TEKENYO LA HOJA Kwa kifupi :

Naamini tunavyokutananavyo katika MAISHA ikiwa ni mpaka hili la KUTONGOZWA na mpaka MWANADADA, ....
....... vifanyacho ni kuamsha TU sehemu ambayo tunayo tayari ndani yetu, ......

......kwa hiyo yule asiyeosha sehemu za siri kabla ya kutongozwa bado ni yule yule wakati ni MUME WA MTU na ana MAKENDE SAFI sikuhizi AU TU anaonekana msafi - katika USWAFI nikiwa na maana sehemu yake ilipalo swala lakujiswafi UTUKUFU imeamka/IMEAMSHWA TU siku hizi lakini alikuwa nayo tokea enzi za wakati habadili chupi wakati hajapata mke CATALYST wa mpaka MAKENDE usafi.

Nakatizia wazo hili HAPA!

Swali:
  • Kwani wewe kama MTANZANIA tokea ukubali mtongozo wa Rais KIKWETE unafikiri URAIS wake umekubadili kitu?
  • Unauhakika ukitongozwa ukakataa tatizo sio tu mtongozaji kakosea kukutongoza LABDA kwa kukupa kauli kibao wakati labda udhaifu wako ni vitendo kama vile vya kuliliwa ndio angalau ujisikie kumpa mtu cheo?


NIMEACHA MKUU na kumbuka HILI NI WAZO TU na lisikutishe hasa kama wewe unaamini kuwa baada ya kutongozwa ukakubali basi ULIBADILISHWA na mahusiano yako na LIMTU lilitokukubalisha.

Au tu nimuachie Ali G na Shaggy katika -Me Julie[Tahadhari:kuna ujinga tani katika video hii kwa hiyo kama uko bize au ni zee la kukwazika unajuachakufanya!]


Au tu General Levy arudishe - Incredible (wicked)

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP