Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kama wewe LEO UNASIFIWA ni MZURI labda CHUKIA swala zima la kuwa kuna KESHO!:-(

>> Wednesday, November 25, 2009

Kesho ni nishai kwa kuwa inaleta katika soko la wazuri ,......
....WAZURI WAPYA.:-(



Na kama maisha ya mtu ni yale yakuuza sura nzuri,.....
....labda chukia KESHO kwa kuwa kila kesho utake usitake yaondoa katika sura yako na mpaka sehemu za siri UPYA!:-(



Swali:
  • Unabisha?

Tushukuru tu kuwa BINADAMU wanamchezo wakujisahaulisha na vitu vya MUDA tu kwa hiyo MTOTO mzuri mwenye machavu mazuri kama embe dodo anawezajisahau mpaka AKASHINDWA KUSTUKIA kuwa wamsifiao sasa hivi WAMEBADILIKA na wampendao sasa HIVI a.k.a washabiki wenye KELELE wanampenda kwa kuwa shavu LA MTOTO MZURI lishageuka na kuwa na mvutio wa embe ng'ong'o nasio tena kama embe dodo .

Na labda tushukuru pia UJANA kwa kusahaulisha vijana ya UZEE.:-(

Swali:
  • Si unajua kila aina ya tako ina mshabiki wake ndio maana kila tako lina mmendeaji hata kama limetepeta?


MTOTO mzuri kama unasikio,...
....JIANDAE KWA SIKU uzuri wako utakapoanza kuongelewa kwa LUGHA ZILIPENDWA a.k.a Lugha imekaa kisentensi -TENSI zilizopita/past tense.

Mfano1. Lile toto liliwahikuwa zuri kweli .:-(
Mfano 2. Mama yenu alikuwa Kijiji kizima kinamtambua kwa kuvutia.:-(


CHakujiuliza:
  • Je uzee sio tu aina ya uzuri?


NIMEACHA WAZO na kumbuka MHESHIMIWA HILI NI WAZO TU!:-(

Na ngojea JOJO aunganishe swala la-Beutiful Girls



Au Christina Aguillera atutie moyo wenye sura mbaya kwa kitu-Beautiful

6 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 12:47 pm  

Hakuna mbaya hapa duniani wote ni wazuri. KAMA CHRISTINA AGUILERA ASEMAVYO "I AM BEUTIFUL NO MATTER WHAT THEY SAY" nakubaliana naye 100%

Simon Kitururu 1:06 pm  

@Dada Yasinta: Nahamu kweli ya kukubaliana nawe na CHRISTINA kama nisingewajua BINADAMU wafikiriavyo.:-(

Kizuri na kitiacho moyo ni kuwa kila mmoja adhaniacho ni kizuri kuna asiyekizimia - kama tu ilivyo kuwa kila mmoja amtamaniye KIUASHERATI kuna LIMTU au Limme lake tu lililomchoka hata kumla denda:-(

Nakuelewa lakini Dada umaanishacho kwa kusema HAKUNA MBAYA hapa DUNIANI kama vile huwezi kutoka baruti bafuni ukilikuta aina fulani la jitu huko linakuchekea.:-(



Swali Kiduchu:

Unataka kusema hakuna limtu ambalo kwa kuliangalia tu sura unajisikia kubadili njia kwa hofu ingawa linakuchekea?

Yasinta Ngonyani 1:26 pm  

Sawa kaka Simon! Ngoja nikuuliza hivi ubaya au uzuri wa mtu ni sura au tabia? Maana mtu anaweza akawa mzuri sana na tabia yake ikawa mbaya kweli. na kinyuma mtu akawa mbaya na akawa na tabia nzuri kweli. Je? lipi ni bara hapo?

Simon Kitururu 3:10 pm  

Naamini Tabia Mbaya kama sura mbaya inategemea na mtazamaji.

Si unakumbuka malaya ajifunzaye UMALAYA tabia nzuri ajifunzazo au - amuigaye tabia nzuri ya kimalaya ni Malaya aliyekubuhu na kufanikiwa kiumalaya?

Nachomaanisha:
Kwa sura kuna ambao mzuri ni Obama na kuna ambao Mzuri ni Dr Remmy.

Kitabia kama wewe ni JAMBAZI na unazimia kazi yako tabia za kilokole kwako si nzuri na kukusababisha tu usiinjoi maisha haya mafupi yaliojaa vitu kibao kiujambazi vifaavyo kuibwa.:-(

Na kama kuna mtu mbaya mwenye tabia nzuri kama wewe ni mpenda sura humchumbii huyo ndio maana unastukia malaya wengi wenye sura nzuri ni wakwanza kuolewa mtaani siku hizi.

Swali:
AU?

Ni kitu mzani tu kati ya Tabia na Uzuri kwa mtazamo wa apimaye mzani kiamuacho ni bora nini.

Kumbuka wenye tabia nzuri sana kwa wengine ni tishio au dalili ya kuna mambo mwenye tabia nzuri hatoi kirahisi eti kwa kuwa ana tabia nzuri.:-(

Yasinta Ngonyani 5:15 pm  

Mmmmmhhhhh:-( Naacha naoga kwenda mbali:-(

Simon Kitururu 10:22 am  

@Yasinta: :-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP